GET /api/v0.1/hansard/entries/949310/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 949310,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/949310/?format=api",
"text_counter": 103,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Sakaja",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13131,
"legal_name": "Johnson Arthur Sakaja",
"slug": "johnson-arthur-sakaja"
},
"content": "Asante sana. Ni vile tu katika hii Bunge hatujakubali sheng . Tungeweza kukubali sheng, ningepeleka watu wa Nairobi na “ radaa” ama na “ rieng”. Lakini sasa kwa sababu sheng haikubaliki ni lazima nijaribu kuzungumza kama Mhe. Faki. Lakini kweli, Benki ya Dunia pamoja na Serikali kuu tumeweza kujenga soko kubwa hapo Kangundo Road. Tayari tumeanza kuona ufisadi ukiingia kwa sababu wale ambao walikuwa wametolewa Outer Ring Road, Mutindwa na mahali pengine--- Kulikuwa na orodha ya wale ambao walikuwa wanapaswa kuwekwa katika soko hiyo lakini inaonekana hizo orodha zimebadilishwa. Ningependa kueleza watu wa Nairobi kuwa hatutakubali hii ifanyike. Wale ambao wanajua wameuza hizo vibanda kwa marafki zao kwa laki tatu wataona! Hatuta kubali hivyo vibanda viende namna hiyo. Ni lazima tuwe watu wa utu na tuwafikirie watu wetu ambao wako hapo chini. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}