GET /api/v0.1/hansard/entries/949312/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 949312,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/949312/?format=api",
    "text_counter": 105,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Sakaja",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13131,
        "legal_name": "Johnson Arthur Sakaja",
        "slug": "johnson-arthur-sakaja"
    },
    "content": "Ya pili, lengo letu kuu la kuleta sheria hii ni kuwapa wale ambao wako katika bunge za kaunti nafasi ya kuiga Mswada kama huu. Tusitoe hii kazi ya kuangalia mambo ya uchuuzi kutoka serikali za kaunti na kuzileta katika Serikali kuu kwa sababu mkiweka vizuizi vingi na mpangilio mkubwa sana wa kuweza kuwasajili hamtakuwa mnasaidia. Mnataka yule mama ambaye ako Kamulu ama Kawangware, aanze kuja hapa katikati mwa jiji la Nairobi kutafuta Mkurugenzi wa idara fulani ili kusajiliwa? Hapana! Mnawasumbua. Wacha watu wafanye kazi walipo. Serikali za magatuzi zinafaa kuenda pahali walipo. Kwa mfano, Serikali ya Jiji la Nairobi inafaa kuenda Kawangware ama Kangemi na kujenga vibanda na kuwaruhusu wafanye kazi. Bw. Spika, kumekuwa na kesi mbalimbali. Nimefurahi kusikia Seneta wa Nyeri akisema kuwa wanaodhulumu wachuuzi lazima wachukuliwe hatua kali. Kuna wakati kulikuwa na shida Eastleigh kulipokuwa na mvutano kati ya Eastleigh BusinessCommunity na wachuuzi. Ukweli ni kwamba kulikuwa na vikundi vya vijana pamoja na askari wa Jiji la Nairobi waliokuwa wanatumia silaha kama nyundo na misumeno kuwapiga kina mama. Hilo ni jambo la kuhuzunisha. Ni kama wachuuzi wamedharauliwa na kuchukuliwa kuwa wahalifu. Sijui kama ni watu wachafu ambao wanafaa kufichwa ndio Jiji ling’are. Jiji litang’araje kama watu hawana ajira ama chakula? Nikitumia mfano kwenye Bibilia, Yesu alisema kuwa ni kama kung’arisha nje ya nyumba ilhali ndani kumeoza ama kuosha kikombe nje na ndani ni kichafu. Tusiwe watu wa kufanya mambo kama hayo. Ni vizuri kupendekeza kuwe na leseni ya mwaka mzima lakini wachuuzi hawana uwezo. Wachuuzi wanafaa kulipia leseni polepole ama kila mwezi. Mchuuzi katika Jiji la Nairobi hawezi kulipa Kshs10,000 ama Kshs5,000 mara moja kwa sababu anahitaji kama Kshs5,000 kununulia vitu anavyohitaji kuuza. Kwa mfano, kuna mchuuzi ambaye hununua ndizi ndiposa auze. Siku hizi wachuuzi hukopa pesa asubuhi kwa njia ya simu kutoka kwa Tala ama Fuliza na kulipa madeni yao jioni. Idadi ya watu wanolipa madeni kila siku ni kubwa sana. Naona Sen. Mutula Kilonzo Jnr. ambaye ni Mwananakamati wa Kamati ya Fedha na Bajeti yuko hapa. Hatupingi biashara za Tala na Fuliza lakini ijulikane kuwa wananyanyasa wafanye biashara. Iwapo unadai riba ya asilimia 20 kila mwezi, inamaanisha kuwa kwa mwaka utakuwa umechukuwa riba ya asilimia 240. Kwa Kiingereza tunasema convertible annually. Hii inamaanisha kuwa mwananchi wa kawaida analipa riba ya asilimia 240 kwa madeni ambayo yanapeanwa na kampuni ambazo hazithibitiwi na Benki Kuu ya Kenya. Maafisa wa Benki Kuu ya Kenya wamesema hakuna sheria za kudhibiti kampuni kama hizo. Kwa hivyo wanapeana tu barua ya “ No objection.” Hata hivyo, mtu kama Bw. Spika au mimi nikienda kutafuta mkopo kwenye benki, nitalipa riba ya asilimia 10. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}