GET /api/v0.1/hansard/entries/949316/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 949316,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/949316/?format=api",
"text_counter": 109,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Sakaja",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13131,
"legal_name": "Johnson Arthur Sakaja",
"slug": "johnson-arthur-sakaja"
},
"content": "Bi. Spika wa Muda, kuna Mswada ulioletwa na Sen. Mutula Kilonzo Jnr. pamoja nami unaohusu jinsi ya kushughulikia mambo ya dharura ama disaster management kwa lugha ya Kiingereza. Mswada huo una pendekeza jinsi ambavyo idara mbalimbali zinafaa kufanya kazi wakati wa dharura. Sote tunafahamu kisa kilichotokea hivi majuzi katika kivuko cha feri cha Likoni. Kuna shirika la Kenya Ferry Services, the Kenya Navy, Kenya Police na Serikali ya Kaunti ya Mombasa. Hata hivyo, watu wanapoteza maisha kwa sababu ya suitofahamu. Leo nimeona video ya gari iliyozama kwenye WhatsApp lakini sijui ulikuwa mto upi. Ghafla watu walikuja na mashua, wakavunja dirisha na kuwanusuru waliokuwa ndani ya gari hilo. Jana tuliambiwa kwamba kisa cha feri ya Likoni kilichukua dakika moja na sekunde ishirini. Kwenye video niliyo tazama leo, walichukua sekunde 60. Lazima kuwe na mashua za kuokoa na wataalamu kwenye kila kituo cha feri kwa sababu jambo lolote linaweza kutokea. Nadhani tunafaa kuwa na Kamati ya Utekelezaji ili Sheria ambazo tunapitisha--- Kulikuwa na haja gani sisi kuleta Mswada ambao sasa uko kwenye sefu ya Hon. Duale katika Bunge la Taifa? Sheria hiyo ingewasaidia Wakenya wakati wa tukio kama hilo. Bi. Spika wa Muda, tunaomba Ofisi yako ifuatilie Sheria ambazo Maseneta wanapitisha hapa. Utapata tunapitisha Sheria nzuri kama hii lakini itachukua miezi sita ua saba huko. Je, itasiadia nani? Tunatumia pesa zinazotelewa na Wakenya kupitia ushuru ilhali hatuwapi huduma ambazo wanastahili kupata. Sisi tuko hapa kuangalia Sheria ambazo zitasadia Wakenya. Ningependa kuambia wachuuzi wa Jiji la Nairobi kuwa tunawafikiria. Nimemwambia Rais na Mawaziri kuwa wanapokutana na the Kenya Private"
}