GET /api/v0.1/hansard/entries/949357/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 949357,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/949357/?format=api",
"text_counter": 150,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Omanga",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13175,
"legal_name": "Millicent Omanga",
"slug": "millicent-omanga"
},
"content": "Ningependa kumwomba Seneta aliyeuleta Mswada huu aone vile ataunganisha na ule wa Wachuuzi Rejareja uliyopitishwa mwaka wa 2015. Hapa Nairobi tumekuwa na shida kubwa sana ya wachuuzi rejareja. Kila wakati utaona wamama, wasichana, na vijana wetu wakikimbizana na askari wa kaunti ambao wanaitwa kanjo. Hawa kanjo wanatumia nguvu zao za kiserikali kuwadhoofisha na kuwahangaisha wafanyabiashara wa jiji la Nairobi. Nairobi ina idadi kubwa sana ya hawa wachuuzi. Bi. Spika wa Muda, nimetembea nchi za nje na nitatoa mfano wa Thailand, ambapo wana soko inayoitwa weekend market . Kila Ijumaa, kuna barabara katikati ya jiji ambayo imetengwa spesheli kwa hawa wachuuzi. Pia, kila jioni kutoka saa kumi na mbili kuendelea usiku mzima, kuna barabara kadhaa katikati ya jiji ambazo zimetengewa wachuuzi. Wale wachuuzi wengine wenye maduka na wale mabwenyeye wanafanya biashara yao mchana. Ikifika saa kumi na mbili wanafunga, kisha wachuuzi rejareja wanakuja na vibanda vyao vya kufungwa. Hivi ni vibanda ambavyo unafungua, unaweka mali yako, unauzia hapo halafu unafunga. Biashara ya weekend market ya wachuuzi rejareja kule Thailand inaleta ushuru kubwa sana kwa Serikali. Hii ni kwa sababu ni soko ambalo limepangwa. Inakuwa rahisi kwa wale wanaochukua ushuru, kama serikali za kaunti. Hii ni kwa sababu kuna sheria ambayo inasema kwamba mahali palipotengwa kuuza bidhaa za soko, biashara itakayofanyika hapo ni ya vitu vya soko pekee. Pia inakuwa rahisi hata kuangalia viwango vya vyakula ambavyo vinauzwa kwenye soko. Inakuwa rahisi pia kwa mnunuzi kwa sababu anajua barabara hii ni ya mboga na hii ya nguo na nyingine ni ya vitu vingine. Bi. Spika wa Muda, kipengee ambacho sikubaliani nacho katika Mswada huu ni kile kinachosema kwamba wachuuzi rejareja wanapaswa kujiandikisha kwa Serikali Kuu. Miji yetu yana matakwa mbalimbali. Siwezi kulinganisha matwakwa ya Jiji la Nairobi na yale ya Mji wa Lamu. Tukisema wachuuzi wetu wote wawe wakijiandikisha kwa Serikali Kuu, basi tunajirudisha nyuma kwa ile shida ambayo ilifanya Bunge la Seneti kuunda Kamati spesheli kuchunguza swala la vifaa vya hospitali. Sote tunakumbuka kuna kamati ambayo imepewa jukumu la kuangalia vile Serikali Kuu iliweza kuagiza vifaa vya hospitali vya kaunti zote. Shida ambayo tumepata ni kwamba iliagiza bila kuangalia mahitaji ya kaunti mbalimbali. Kuna kaunti ambazo tayari zilikuwa zimenunua hivyo vifaa lakini zililetewa hivyo vifaa. Unapata kuwa kaunti ambayo haina nguvu za umeme na maji, inaletewa vifaa ambavyo vinatakiwa kutumia umeme. Kazi hii ingeachiwa kaunti yenyewe ijifanyie; wangejua kama hatuna umeme, wacha tununue kifaa ambacho kinaweza kutumia jenereta ama mafuta ya diseli. Kwa hivyo, kuweka sharti katika sheria hii kuwa wachuuzi waende kujiandikisha kwa Serikali Kuu itakua ngumu kwa sababu kila jiji inaelewa wafanyakazi wake. Kazi hiyo ingeachiwa kaunti yenyewe kwa sababu tuko kwa serikali ya ugatuzi. Tungewacha kaunti yenyewe na bunge lake kutengeneza zile sharia ambazo wale wafanyabiashara wanapaswa kufuata. Bi. Spika wa Muda, unapata kuwa wachuuzi wengi ni akina mama na vijana. Mara nyingi akina mama huenda sokoni na watoto wao. Wakati huu, kaunti nyingi The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}