GET /api/v0.1/hansard/entries/949358/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 949358,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/949358/?format=api",
    "text_counter": 151,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Omanga",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13175,
        "legal_name": "Millicent Omanga",
        "slug": "millicent-omanga"
    },
    "content": "zinapoteza pesa za ushuru kwa sababu biashara hii haijawekwa kwa mpango. Nitapeana mfano wa Nairobi kwa sababu ndipo ninaishi na hapo ndiyo naelewa zaidi. Utapata jioni wachuuzi wanafanya biashara yao ni kama wanaiba kwa sababu hawajawekewa mpangilio wa kufanya kazi yao. Wanakaa wakiangalia kama kanjo anakuja na pia kuna watu ambao wanakuja kuwadanganya kwamba kanjo wanakuja. Unapata mama anabeba vitu vyake, nyanya zake zinaanguka na anapoteza vitu vingi sana. Wakati mwingine wale kanjo wanapokuja wanashika yule mama na kumpeleka kortini. Ni aibu kubwa wakati mwingine akina mama hao wanabakwa hapa Nairobi. Kwa sababu ya hio, Kaunti ya Nairoi haiwezi kukusanya ushuru kutoka kwa hawa wafanyabiashara. Hata wafanyabiashara wakiuza, utapata kwamba hawa kanjo hawawezi kukusanya ushuru kwa sababu hawana wakati wa kukaa na yule mfanyabiashara ili awezekulipa ushuru. Bi. Spika Wa Muda, nigependa kuunga mkono Mswada huu na kumuomba aliyeuleta aweze kuangalia swala la uhusiano wa Serikali Kuu na serikali za kaunti. Asante, Bi. Spika wa Muda."
}