GET /api/v0.1/hansard/entries/949477/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 949477,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/949477/?format=api",
"text_counter": 72,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mvita, ODM",
"speaker_title": "Hon. Abdullswamad Nassir",
"speaker": {
"id": 2433,
"legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
"slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
},
"content": " Asante, Bwana Spika. Wakati mwingine ulitoa amri ya kuwa kwa vile niko katika Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma, itakuwa si sawa kuyazungumza yale ambayo yanazungumzwa ndani kabla hayajakithiri zaidi. Naomba nipewe ruhusa kuzungumzia jambo moja tu. Katika Ripoti ya Auditor-General ya 2016/2017 alitaja hili jambo na akasema kuwa hizi pulleys nyingi sana za hizo ferry hazifanyi kazi. Alielekeza ya kuwa hizi ferry ni hatari ambayo iko njiani. Baada ya pale, kuna barua zilizopelekwa kwa Wizara. Kwa sababu ya nyadhifa ambazo Bunge ilinipatia kama Mwenyekiti, sitoweza kuyazungumza sana sasa hivi mpaka niilete ile ripoti. Naomba wenzangu ya kuwa ile ripoti ikija, haya mambo yatakuwepo ndani yake. Na yakiwepo, ni muhimu ile Kamati ya kufuatiliza ifanye hivyo ili wale ambao walihusika na wakaambiwa kuwa athari fulani iko njiani…"
}