GET /api/v0.1/hansard/entries/949487/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 949487,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/949487/?format=api",
    "text_counter": 82,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lungalunga, JP",
    "speaker_title": "Hon. Khatib Mwashetani",
    "speaker": {
        "id": 2163,
        "legal_name": "Khatib Abdallah Mwashetani",
        "slug": "khatib-abdallah-mwashetani"
    },
    "content": " Asante sana Mheshimiwa Spika. Kwanza, jambo la kusikitisha ni kuwa ukiangalia sababu ya wao kutoweza kulitoa lile gari pale lilipozama ni kwa sababu wameshindwa kupeana hewa ya kununua ambayo itakwenda mita 60 chini. Hewa walionayo ni ile ambayo inaweza kwenda mita 30 chini. Kule sehemu tunazotoka kama Vanga, kuna vijana ambao ni wenyeji wazoefu na wanaweza kwenda mita kama 60 chini na wakakaa kama masaa mawili bila kuwa na oxygen ya kununua. Sababu ya mambo kama haya kutokea ni pengine wale wanaoajiriwa pengine wana uzoefu wa kuogolea kwenye mabwawa au swimming pool lakini hawana uzoefu wa kuogelea kwenye maji. Mbali na hivyo, ile sehemu ya Likoni ambayo tunaizungumzia ni sehemu ambayo ina papa. Nafikiri kila mmoja ana utamu wa roho yake. Ikiwa umekuzwa katika hali ya kuwa uko ndani ya bahari kila siku, basi nina imani ni sawa na maasai ambaye yuko kichakani. Maasai anaweza kuwa amesimama hapa, simba yuko pale na hana wasiwasi. Mimi na wewe ambao hatujazoea, tukiwa ndani ya gari na simba yuko nje, tuko na wasiwasi. Ni kama yule diver ambaye amezoea na hakusoma kufika Form Four lakini ana uwezo wa kuingia pale ndani akasaidia janga kama lile. Ni muhimu sana tulipatie nafasi jioni ili tulizungumzie kindani na liweze kueleweka."
}