GET /api/v0.1/hansard/entries/949704/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 949704,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/949704/?format=api",
"text_counter": 299,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Niliuliza vijana kule Lamu vile wangefanya wangekuwa karibu na ile feri lile tukio likifanyika na jibu lao ni wangechukua kamba kwenye feri, waruke na kulenga kuifunga lile gari. Je, kufunga kamba kwenye lile gari liliwashinda vijana wenye vyeti ilhali vijana wengi walio na ujuzi wamekaa tu kule mtaani na kizingitini? Watoto wetu sasa wamechoka na wamesema wenye vyeti sasa wafanye kazi. Naeza kukueleza ni kina nani kizingitini wanaeza fanya hiyo kazi ya diving haraka. Tunayo Adhamani Mbarauzi, Lali na wengineo wengi chap chap hata wanaeza fika ishirini. Lakini, mkitangaza nafasi za kazi, mtachukua runners muwapeleke pale nasisi tukuwe watu wa kupanda kofi. Basi, wazamie na wao pia wafanye ile kazi kwa sababu sisi watu wa Lamu hatuwezi kusema tupelekwe tuwakilishe Kenya kwa mbio. Nchini Kenya kuna wanaokimbia – Sisi hatuwezi kazi hiyo. Jamani, hayo maji hamuyawezi. Msitafute hizo nafasi za kazi mkaua watu maana wale waliochukua zile kazi ndio walioua wale. Mhe. Naibu Spika wa Muda, pale kwetu hiyo ni kazi ndogo sana. Lakini, mtakapo advertise nafasi za kazi kule Coast Guard, mtaona wengi wakidai zile nafasi. Ingekuwa rahisi Serikali iwape njia... Mkitaka kuandika kazi kwenye Navy ama Coast Guard, mseme tu walete vijana wa vizingitini. Inabidi tu muwaingize kweny feri na mkiwa katikati ya bahari, muwaambie waruke muone vile watafanya kwanza ndio waandikwe. Wale walioko pale kwa sasa, natoa challenge kwao. Tuwachukue wao nao tuwarushe pale baharini ili tuone ni kina nani watafanya ile kazi. Mhe. Naibu Spika wa Muda, ni mambo ya kusitikisha.Watoto wetu wanachukua pweza wakienda kuzamia ndani mita hata sitini bila kutaka gesi wakiendea kamba ambayo kwa lugha ya kizunguni ni lobster. Ni kitu wamezoea. Wanachukua jahazi na kuelekea kule deep sea kuvua samaki. Wakifika pale, wanaruka na kuacha jahazi na mtu mmoja. Kuna watu wamezoea zile kazi jamani. Hapa, tutalaumiana eti Kenya Ferry Services, Coast Guard, Kenya Navy... Kenya Ferry Services yenyewe yafaa iwe na kitengo chao. Wale mabouncer mumewachukua waende disco maana sio kazi yao –hawawezi ile kazi. Wangelikuwa wanaweza, ile kazi ndogo tu ya juzi... Mmoja angejirusha akiwa amebeba kamba na kuifunga lile gari na wangesave maisha. Mpaka sasa, kutoa gari imewashinda ilhali siyo kazi kubwa. Inabidi uende na mitungi ya 200 litres ya fuel kule chini, uifunge ile gari na litatoka lenyewe. You do not need rocket science. Kazi hiyo itakuwaje mpaka sasa hivi bado haijafaulu? Inasikitisha ya ukweli. Jamani, wacha tufanye kazi. Hizo certificates hazitupeleki mahali maana skills pia ni muhimu. Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda."
}