GET /api/v0.1/hansard/entries/949707/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 949707,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/949707/?format=api",
    "text_counter": 302,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Wundanyi, WDM-K",
    "speaker_title": "Hon. Danson Mwashako",
    "speaker": {
        "id": 13509,
        "legal_name": "Danson Mwashako Mwakuwona",
        "slug": "danson-mwashako-mwakuwona"
    },
    "content": " Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuunga mkono Hoja hii ambayo dada yangu Mhe. Mishi wa Likoni ameleta Bungeni. Maswala haya tunayoyaongelea hapa kama Bunge la Taifa ni maswala mazito. Tunaongelea swala la mmoja wetu na mtoto wake kupoteza maisha. Kwanza, naomba Mwenyezi Mungu aziweke roho za hao watu wawili mahali pema peponi. Aibu kubwa imetupata kama nchi. Mimi nimekuwa nikipiga mtazamo kuwa mambo haya yangetokea katika nchi zilizoendelea, taifa jirani kama Tanzania ama mahali ampapo kuna vijana ambao dada yangu kutoka Lamu amewataja na wapewe ruhusa ya kufanya kazi mahali kama pale, leo hii hatungepoteza roho hizo mbili. Asubuhi kulikuwa na Mswada hapa wa kuongeza hukumu ya wale ambao wanafanya ufisadi. Mswada ule, kwa mtazamo wangu, ni Mswada uliokuja wakati mzuri. Haya tunayoyajadili ni mazao ya ufisadi nchini Kenya. Tumwekuwa wafisadi kufikia kiwango cha kwamba hata kifo hatukiogopi. Ufisadi umetufikisha pale ambapo watu wafa maji ilihali kuajiri mpiga mbizi ni rahisi kwa malipo yake, kuliko kupeana zabuni kwa kampuni zinazoweka usalama pale Feri. Ukienda kule Feri, utapata kuna wanaume waliokula wakashiba. Wako pale wakijitapa. Mkasa huu umetuonyesha kuwa hawana kazi pale. Badala ya kuandika kazi watu ambao wanaweza kuokoa maisha, Feri na Bodi yake yote imeona ni vyema ipeane zabuni na kandarasi kwa vitu ambavyo si vya msingi. Maisha ni kitu ambacho ni lazima tukilinde. Juzi nilimwona Mkurugrnzi akisema kwamba hawana wapiga mbizi. Mara wanasena hawana gesi ya kushuka chini ya maji kizitoa zile miili. Ufisadi umemaliza nchi hii. Ni wakati mwafaka kwa Bunge hili la Taifa kusema ni lazima tupigane na ufisadi kwa njia zote tukianza na Kenya Ferry na kwingineko. Hata mahospitalini watu wafa kwa sababu ya ufisadi. Wapiga mbizi wanajeshi walioko pale Mtongwe, kama kilomita moja ama mbili kutoka pale Feri, wana tajiriba. Wanatambulika dunia nzima. Lakini, hakukuwa na mawasiliano baina ya Kenya Ferry na wao kuwatoa waje kuokoa maisha. Hili ni jambo la kusikitisha. Leo, tumewapoteza watu wawili katika janga lile. Si mara ya kwanza tumepoteza watu pale. Pale ni eneo Bunge la Mhe. Mishi Mboko. Ni lazima tupatiwe ripoti kamili ya kile kinachoendelea ndani ya Kenya Ferry. Tumechezewa ya kutosha. Kila mara kinachofanyika pale ni njia ya watu kujitajirisha. Tulitarajia wakati kama huu Waziri... Ingelikuwa ni maswala mengine yametendeka kwingineko, Waziri wa Uchukuzi angekuwa amefika mahali pale. Leo hatujamwona Waziri. Tumemwona Mwenyekiti tu, Mwazo..."
}