GET /api/v0.1/hansard/entries/949756/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 949756,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/949756/?format=api",
    "text_counter": 351,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kisauni, WDM-K",
    "speaker_title": "Hon. Mbogo Ali",
    "speaker": {
        "id": 13383,
        "legal_name": "Ali Menza Mbogo",
        "slug": "ali-menza-mbogo"
    },
    "content": "Kwanza, ninatoa pole zangu kwa jamii ya marehemu Mariam na mtoto Amanda na kujulisha Bunge hili, ijapokuwa walifariki katika kivuko cha Likoni, ni wakazi kutoka eneo la Bunge langu la Kisauni na hivi tunavyozungumza, tumeanza mipango ya kuchanga pesa katika kusaidia mazishi. Kwa hivyo, ninaomba Wabunge wenzangu pia tuweze kusaidiana kwa njia moja au nyingine. Wale wataweza kuchanga, tutashukuru zaidi ili tuweze kufikisha msaada ule kwa jamii ambayo imepata mkasa huu."
}