GET /api/v0.1/hansard/entries/949757/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 949757,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/949757/?format=api",
"text_counter": 352,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kisauni, WDM-K",
"speaker_title": "Hon. Mbogo Ali",
"speaker": {
"id": 13383,
"legal_name": "Ali Menza Mbogo",
"slug": "ali-menza-mbogo"
},
"content": "Kwanza kabisa, hili ni janga la kitaifa. Ni janga ambalo limeonyesha udhaifu mkubwa kwa taifa la Kenya. Ni aibu ikiwa mkasa huu ulitokea siku ya Jumapili jioni na mpaka leo, mili haijatolewa. Jumapili ilikuwa ni tarehe 29 mwezi wa tisa, leo tumefika tarehe mbili mwezi wa kumi, siku tatu, na mpaka sasa tunavoongea, hakuna kitu ambacho kimepatikana. Imetuonyesha udhaifu kuwa kama taifa hatuko tayari kupambana na majanga kama haya. Ijapokuwa wakati tokeo la kihuni la wale magaidi litakapotokea katika sehemu hiyo, tutaona vitengo vya usalama vinavyohusika kupambana na magaidi vinavyojitahidi. Lakini leo, jeshi letu la wanamaji limeonyesha udhaifu mkubwa. Wamefundishwa na wanaujuzi wa kushugulikia maswala ya ndani ya maji. Lakini, kwa siku tatu wameshindwa kuokoa wale maiti ambao wako pale ndani na kutoa gari iliyozama katika kivuko cha Likoni. Kama Taifa, hii imetuonyesha hatuko tayari kabisa. Kivuko kile cha Likoni kinavukisha magari elfu sita na watu zaidi ya laki tatu kwa siku. Je, ingekuwaje kama kwa bahati mbaya feri ile ingezama? Ikiwa tukio la mtu mmoja limetushinda. Je, kama feri ile ambayo inabeba watu elfu nne mia tano wakati inavukisha kwa safari moja ingezama? Je, tuko tayari kwa swala kama The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}