GET /api/v0.1/hansard/entries/949758/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 949758,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/949758/?format=api",
"text_counter": 353,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kisauni, WDM-K",
"speaker_title": "Hon. Mbogo Ali",
"speaker": {
"id": 13383,
"legal_name": "Ali Menza Mbogo",
"slug": "ali-menza-mbogo"
},
"content": "hilo? Hatuko tayari. Hii imetuonyesha tuko na kazi ya kufanya na kama taifa ni lazima watu wawajibike. Ningekuwa Waziri anayehusika na maswala ya usafiri ningekuwa nimewacha kazi kuonyesha imenishinda. Mkurungezi mkuu wa Kenya Ferry, Bw. Bakari Gowa angekuwa tayari ameenda nyumbani na yuko korokoroni. Haya ndio mambo yanayofanyika katika nchi zilizoendelea. Maisha ya Mkenya mmoja ni sawa na kupoteza umma mzima. Huyu ni mama na mtoto wake. Ukiangalia mwaka wa 1994 katika kivuko cha Mtongwe tulipoteza maisha ya Wakenya 272, na kivukio kile kiko mita 40 kutoka kambi ya wanajeshi wa maji. Hiyo feri ilikuwa imebeba watu 400. Watu 128 waliokolewa na wavuvi na wapiga mbizi wa mtaani. Lakini kikosi cha Kenya Navy kilishindwa kuokoa maisha. Leo imetuonyesha vilevile udhaifu walionao. Mashirika ya Kenya Ports Authority (KPA), Kenya Maritime Authority (KMA) na Kenya Coast Guard Services (KCGS) ni vitengo tunapatia pesa nyingi. Tunajua pesa tunazopitisha katika maswala yetu ya bajeti katika mambo ya usalama. Ni pesa chungu nzima tunazopatia pande lile. Lakini, leo wameshindwa kuokoa gari moja na maiti zilizo ndani kwa siku tatu mfululizo. Hili ni jambo ambalo linatusikitisha sana kama watu wa Pwani, Mombasa na Jamhuri ya Kenya. Tukiangalia yale ambayo yametokea, ninafikiri kuna umuhimu ile Kamati ya Usafiri iweze kushugulikia swala hili na kulete ripoti hapa katika Bunge la Kitaifa ili tupate kujua kiini cha kilichotokea na kusababisha ajali ile. Pia, kitu gani kitafanywa kwenda mbele ili tusije kupata madhara makubwa. Kitu ambacho tunaangalia sasa ni kwamba tutakuja kupata majanga makubwa ambayo tutashindwa kujiondoa kama taifa. Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda."
}