GET /api/v0.1/hansard/entries/949765/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 949765,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/949765/?format=api",
    "text_counter": 360,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kaloleni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Paul Katana",
    "speaker": {
        "id": 13357,
        "legal_name": "Paul Kahindi Katana",
        "slug": "paul-kahindi-katana-2"
    },
    "content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Kwa niaba ya wakazi wa Kaloleni, ningependa kutoa rambirambi zangu kwa jamii ya mama Mariam na mtoto wake Amanda. Ni jambo la aibu sana katika nchi hii kuona kwamba mtoto na mamake wanapoteza maisha kwa uzembe wa watu ambao walitwekwa jukumu la kutoa huduma katika nchi hii. Inaonekana Wakenya hatuko tayari kuona kwamba kukitokea janga tunaweza kusaidia wananchi wetu. Kuna vijana ambao wanauzoevu wa kupiga mbizi katika eneo la Likoni. Lakini ni jambo la kushangaza kwamba hawajapatiwa nafasi ya ajira katika Shirika hili la Kenya Ferry. Tumekuwa tukiajiri watu kwa sababu ya makaratasi tunasema wamesoma. Lakini kuna wale hawajasoma na wanauzoevu wa kupiga mbizi kama kijana anayeitwa Musa. Amekuwa akiokoa maisha ya watu na sasa ameomba kazi kwa Shirika la Kenya Ferry kwa miaka zaidi ya kumi na tano na hajapata ajira. Tungekuwa tumewapatia hawa vijana nafasi wangeweza kuokoa maisha ya wananchi katika feri. Tumeona kwamba hatuwezi kusaidia kukitokea janga. Pengine shule iungue. Je, tuko tayari kusaidia wananchi wetu? Kumekuwa na Tume ambayo lilibuniwa baada ya ajali ya Mtongwe. Tulijifunza nini kutoka kwa ile Tume? Jambo la kusikitisha ni kwamba jeshi letu la wanamaji, ukipita kwa feri, utaliona linafanya mazoezi ya maandalizi ya Mashujaa Day. Sasa wanapita pale na hawawezi kuokoa maisha ya yula mama na mtoto wake. Utaona tarehe 20 Rais akiwa pale utaambiwa hiki ni kikosi maalum cha wapiga mbizi. Sasa tujiulize, wanapiga mbizi wapi. Wanapiga mbizi kwa bwawa la maji au kwa bahari. Itakuwa aibu hata kwa Rais kuwakubali wapiga mbizi ambao tutawaona tarehe 20 kupita mbele yake kwa sababu wameshindwa kuwasaidia wananchi ambao walistahili kusaidia. Gari lilielea kwenye maji kwa muda wa dakika 20 lakini unasikia sasa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Feri anasema hakuna wapigambizi ama wapigambizi hawana hewa ya kuingia baharini. Hii ni aibu kubwa kwa shirika kama hili. Umefika wakati Bunge hili lichukue hatua za kisheria dhidi ya watu hao ambao wanazembea katika kazi zao. Hata tukisema wananchi wafidiwe, hatuwezi kuokoa maisha yao. Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda."
}