GET /api/v0.1/hansard/entries/949770/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 949770,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/949770/?format=api",
"text_counter": 365,
"type": "speech",
"speaker_name": "Magarini, ODM",
"speaker_title": "Hon. Michael Kingi",
"speaker": {
"id": 13412,
"legal_name": "Michael Thoyah Kingi",
"slug": "michael-thoyah-kingi"
},
"content": " Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi ya kuchangia mada hii ya leo. Kwanza, ninatoa pole zangu kwa familia ya mwendazake, Mariam, pamoja na msichana wake Amanda. Nikiwa nimesimama hapa, nimejawa na huzuni kutokana na tukio ambalo ni lazima kama Wakenya au Wajumbe katika Bunge letu tujiulize maswali. Je, jambo kama hili lishawahi kutokea mwanzoni katika kivuko cha Likoni? Ukiangalia, ni kweli lishawahi kutokea. Je serikali imechukua hatua gani. Ukiangalia kwa kina zaidi utagundua kwamba ijapokuwa majanga haya yanatokea mara kwa mara katika kivuko cha Likoni utaona kwamba Serikali haijatilia mkazo katika kuhakikisha kwamba majanga kama haya yanapotokea watu wanaweza kuokolewa. Jambo la pili tunafaa tujiulize ni ajali kama hii ikitokea, je watu wangeweza kuokolewa? Ukiangalia, katika ajali hii The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}