GET /api/v0.1/hansard/entries/949771/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 949771,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/949771/?format=api",
    "text_counter": 366,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Magarini, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Michael Kingi",
    "speaker": {
        "id": 13412,
        "legal_name": "Michael Thoyah Kingi",
        "slug": "michael-thoyah-kingi"
    },
    "content": "ingekuwa rahisi kabisa kuokoa watu lakini idara inayohusika ya uchukuzi haijajitayarisha mwafaka kuhakikisha kwamba majanga kama haya yakitokea watu wanaweza kuokolewa. Ninajiunga na Wabunge wenzangu ambao wamesema kwamba feri nyingi hazina vizuizi mbele na nyuma ya feri. Unapoingiza gari lako pale utaona mbele kuko wazi na hakuna kizuizi na gari inaweza kusukumwa mbele ikaingia kwa maji ama ikarudi nyuma na ikaingia kwa maji. Hili ni jambo ambalo Kenya Ferry au idara husika ya uchukuzi ingetilia maanani kuweka vizuizi. Haigharimu pesa nyingi lakini kwa sababu hawajaona umuhimu wa maisha ya wananchi wa Kenya ninafikiri ndio maana wanaishikilia legelege. Wakati huu waziri anayehusika inapaswa saa hii tunapozungumza ndani ya Bunge hili tayari awe amejiuzulu. Kama hatafanya hivyo, mimi ninamuomba Mheshimiwa Rais ikiwezekana amchukulie Waziri hatua. Hatua ya kwanza ambayo inafaa kuchukuliwa huyu Waziri ni kuhakikisha kwamba ameachishwa kazi. Ninamuomba Mheshimiwa Rais alitekeleze ombi hili. Tunaweza kumlaumu mkurugenzi wa ferry. Kwa sasa siwezi kusema kwamba ninamlaumu kwa sababu sijui kama alikuwa anapeleka mapendekezo haya kwa Wizara inayohusika na kama alikuwa anapata msukumo kutoka kwa idara inayohusika. Kwa hivyo ikibainika pia kwamba mkurugenzi mkuu huyu labda alikuwa anapendekeza ama hapendekezi mwafaka ambao unatakikana kufanyiwa katika feri hizi, basi yeye pia hana budi ajiuzulu. Hali ya majanga Kenya hii imekuwa ikitokea mara kwa mara. Lakini ni kama Serikali haiko tayari. Mfano mbali na huu, katika eneo Bunge langu, juzi kulitokea janga la mafuriko. Watu wengi waliokolewa na raia. Wale wahusika walikuja pale baada ya siku tatu. Mtu akizama maji tayari ufa kabla ya siku tatu. Mheshimiwa Rais ana ile kalamu ya kuandika na kufuta. Naomba Mheshimiwa Rais awachukulie hatua mwafaka wahusika wote ambao wameaminika kutunza maisha ya wananchi na hawafanyi hivyo. Kwa hayo, naomba tujiunge na familia ili tuomboleze vifo hivyo."
}