GET /api/v0.1/hansard/entries/949776/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 949776,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/949776/?format=api",
"text_counter": 371,
"type": "speech",
"speaker_name": "Rabai, ODM",
"speaker_title": "Hon. William Mwamkale",
"speaker": {
"id": 2672,
"legal_name": "William Kamoti Mwamkale",
"slug": "william-kamoti-mwamkale"
},
"content": " Asante sana, Bwana Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii. Nitaanza kwa kutoa rambirambi zangu kwa niaba ya wakaazi wa Rabai kwa familia ya mama Mariam na msichana Amanda. Tuna imani kwamba Mungu atawaweka mahali pema peponi kule wameenda. Ukweli wa mambo ni kama wenzangu walivyozungumza. Janga hili la feri limesababishwa na wafanyikazi wazembe, watu ambao hawataki kuchukua majukumu yao kama inavyotakikana. Tunajua kwamba kuna mgao wa pesa unaopatiwa kila shirika. Shirika la Feri kama mashirika mengine inagawiwa pesa. Ukienda Likoni sasa hivi ama ukiwa mjini Mombasa, utaona magari mazuri mazuri ya Kenya Ferry. Utaona barabara pale karibu na ofisi zao zinang’arishwa. Lakini umuhimu wa Kenya Ferry ni kuangalia usalama wa watu wanaotumia kivuko kile. Tunajua sasa hivi tutaambiwa kuwa tume imeundwa kuchunguza ni nini kilisababisha ajali ile. Lakini kila kitu kiko wazi kwa sisi ambao hutumia feri ile. Mimi mwenyewe nimewahi kuvuka na ile feri si mara moja au mbili. Mnafika mwisho wa safari kisha mnaambiwa feri mpaka irudi kinyumenyume, igeuke ndio iweze kushukisha abiria ama watu. Sababu ni kwamba milango haifanyi kazi. Feri ikiwa nzima au katika hali yake ya kisawasawa, huwa baada ya watu na magari kuingia ndani, milango ya feri inainuka na kufunga vizuri kiasi cha kuwa hata mtu akisukumwa hawezi kutoka nje au gari ikishuka kwa sababu pengine kwa sababu brakes zimekataa, halitaweza kufika nje, litagongwa na vizuizi na kuzuiwa na milango. Lakini katika feri zetu milango yote haifanyi kazi. Kufanya tu marekebisho ya milango imeshinda wakurugenz, imeshinda wafanyikazi wa Shirika lile. Naunga mkono wenzangu kwamba kama mtu hawezi kazi, msituharakishe kwenda makaburini. Msihatarishe maisha ya watu 6,000 wanaotumia feri ile kwa siku moja. Hapa ni mahali ambapo Serikali ingeangalia vizuri na kuhakikisha watu wake wanalindwa. Wapigaji mbizi ni muhimu kwa Shirika kama lile. Inakuwaje kuwe hakuna wapigaji mbizi na tunajua chochote chaweza tokea ndani ya maji? Hili janga lilitupata 1994 na tulitarajia kwamba kungekuwa na mikakati kufikia sasa. Wakenya hungoja mpaka kitu kitokee; sio kwamba haikuonekana mambo haya hayatatokea. Juzi kule Rabai, nimekuwa na ajali mbaya sana. Tumepoteza watu tisa mahali pamoja. Mahali pale tumeomba matuta yajengwe na Kenya Rural Roads Authority (KeRRA) na Kenya National Highways Authority (KeNHA), wakazembea kazi mwisho, tuakaambiwa KeRRA ndio wamepewa ile kazi mpaka watu wakaangamia. Sisi tuanambia wanaochukua majukumu ya The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}