GET /api/v0.1/hansard/entries/949780/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 949780,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/949780/?format=api",
"text_counter": 375,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kinango, ODM",
"speaker_title": "Hon. Benjamin Tayari",
"speaker": {
"id": 13379,
"legal_name": "Benjamin Dalu Stephen Tayari",
"slug": "benjamin-dalu-stephen-tayari-2"
},
"content": "Kusema ukweli, wafanyi kazi wengi wa feri hawana tajiriba ambayo inatakikana kuhakikisha kwamba wanafanya kazi ile vizuri. Wiki mbili zilizopita kabla ya ajali hii kutokea, feri moja ingegongwa na meli ambayo ilikuwa inapita. Watu wa feri walisema ya kwamba wanajua wanafanya nini na walikuwa tayari kwa lolote. Lakini kusema ukweli, ni Mwenyezi Mungu ambaye aliokoa ajali ile. Tungepoteza watu wengi sana pale Likoni wiki mbili zilizopita. Vile alivyosema mwenzangu, mwaka 1994 tulikuwa na ajali pale Mtongwe ambapo tulipoteza watu wengi sana. Ajali hiyo ilikuwa mita kadhaa na pale ambapo maafisa wa Kenya Navy wanaishi ama wanafanyia mazoezi yao lakini hakuna lolote walifanya mpaka tukapoteza watu wengi. Juzi tulipoteza dada yetu kilomita moja tu kutoka pale maafisa wa Kenya Navy wanakaa. Wakati gari lilikuwa linatokomea chini, walikuwa wanafanya mazoezi hapo wakizunguka kwa boti zao. Wao hufanya starehe hapo badala ya mazoezi. Najiuliza na nauliza wenzangu, hizi nguo nyeupe ambazo wale wenzetu wamepatiwa ni za kuonyesha kwamba haziingii uchafu ama ni za kufanyia kazi? Naona hakuna kazi yoyote wale ndugu zetu wanafanya pale kwa Kenya Navy."
}