GET /api/v0.1/hansard/entries/949799/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 949799,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/949799/?format=api",
"text_counter": 394,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lungalunga, JP",
"speaker_title": "Hon. Khatib Mwashetani",
"speaker": {
"id": 2163,
"legal_name": "Khatib Abdallah Mwashetani",
"slug": "khatib-abdallah-mwashetani"
},
"content": "kuongoza katika shirika lolote, yeye kama mkurugenzi anatakikana apange mikakati ya kisawasawa na kuangalia vitengo ambavyo haswa vinatakikana vipewe kipaumbele katika mipango yake ya kuhakikisha anaendesha shirika lile. Lile gari ambalo lilizama pale lilichukua karibu dakika 30. Wale wanajeshi wa Navy waliokuwa wakifanya mazoezi waliona likizama. Kama baharia – mimi uogelea – na ikiwa hujazoea hata kama wajua huna vifaa hauwezi kuruka kwenda kusaidia. Kwa hivyo, mimi kama Mbunge nilizungumza na wenzangu kule Vanga na hii leo tunavyozungumza, katika timu ambayo inazunguka na imeruka kule chini kuhakikisha wametoa miili, ni vijana wanne ambao hawakusoma, hawana elimu lakini kazi yao ni kuruka ndani ya maji na kuhakikisha wametoa vilivyo kule chini. Kwa hivyo, suala la kuajiri wafanyakazi haswa katika hivi vivuko ambavyo vinatumia madau ni lazima tuweke katika sheria kuwa katika hivi vivuko, lazima kuwe na watu wawili au watatu ambao wana tajiriba ya kisawasawa na ile ari ya kuingia kule ndani kusaidia wakati wowote. Hili ni swali ambalo sisi tunajiuliza kama wakenya: Basi sisi kama Wakenya ikiwa hatuwezi kubuni basi kuiga pia hatuwezi? Ukiangalia nchi za kuendelea ambazo tunategemea kuiga mipango yao, katika kila sehemu hata zile sehemu ambazo vijana wetu wanakwenda kujivinjari za bichi, huwa tumeweka walinda usalama. Kukitokea janga lolote, wanaweza kuingia pale na kusaidia kwa haraka. Kwa hivyo, ombi langu, mbali na kuwa hili suala limekuwa suala nyeti, wale wote ambao wanahusika, sio kuhusika kwa kuwa walitenda, lakini kuhusika kuweka mipango kabambe, wajiuzulu ama Rais wa Jamhuri ya Kenya aseme kila mmoja ambaye amezembea kikazi ni sharti kukitokea jambo kama hili ajiuzulu. Hii italeta heshima katika haya mashirika ambayo yamepewa nafasi ya kuongozwa na watu. Vilevile, nikienda upande wa usimamizi, leo ukiangalia sehemu kama ile, unakuta wakati feri inatakikana kushukisha, kabla gari halijatoka wananchi hupita. Leo ni baharini kesho utasikia kuna wananchi wamepandiwa na magari. Hii yote ni kwa sababu ya ukosefu wa usimamizi bora. Ikiwa hakuna usimamizi bora, majanga yataendelea kutokea. Vilevile, ukiangalia uajiri wa watu, ukiajiri mkurugenzi, lazima awe na tajiriba ya usimamizi. Ukichukua mkurugenzi ambaye ni mhasibu au mhandisi, lazima awe na tajiriba ya usimamizi ili ajue kuna masuala kama inventory, masuala ya kuangalia spares za hiyo meli zinatoka wapi. Tulitoa shillingi billioni 1.8 kununua feri mbili. Ile feri ya kwanza ambayo ililetwa, azimio lilikuwa ni feri mpya, lakini iliyoletwa ilikuwa ishatumika. Kwa nini tutumie vifaa ambavyo vimeshatumika katika nchi zingine na hali tunaweka pesa za kisawasawa kuhakikisha tumepata feri za kisawasawa na zile pesa tumetoa ziwe ni haki kwa mwananchi ili apate huduma ya kisawasawa? Pili, hadi wa leo hizo feri hazijafika, hatujui pesa zimeenda wapi. Kama Bunge la Kitaifa, hayo ni maswala ambayo ni muhimu tuyaangalie kwa undani."
}