GET /api/v0.1/hansard/entries/949804/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 949804,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/949804/?format=api",
    "text_counter": 399,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ali Sharif",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": " Asante Naibu Spika wa Muda. Kwanza kabisa, ningependa kuungana na wenzangu kutoa rambirambi zangu za pole kwa familia waliopoteza wapendwa wao.Vile vile, ningependa kumpongeza Mhe. Mishi kwa kuileta Hoja hii Bungeni. Naibu Spika wa Muda, Waheshimiwa wengi wamezungumza kwa masikitiko makubwa na kwa kuzingatia yaliyojiri kutokana na kisa hiki cha hivi majuzi cha kupoteza ndugu zetu Wakenya katika mkasa wa feri. Vile vile, ni masikitiko makuu kwa Wakenya. Ni majonzi makubwa kwamba, hata baada ya tukio hili, mpaka sasa, hakuna juhudi zozote ambazo zimefanywa kusawazisha hii mahali. Kwa kweli, ni masikitiko makubwa, na ni aibu kwa nchi hii kwa jumla. Naibu Spika wa Muda, tatizo kuu la Kenya ni kwamba tunasahau na hatuna ile imani ya kusikitikiana, na kadhalika. Ingawaje kifo kitamfikia kila mmoja wetu, na kila mtu ako na siku yake ya kufa, majanga na vifo vingine husikitisha. Kwa hakika, ni aibu kubwa kwa Serikali yetu. Leo hii, Serikali inazidi kuendesha zoezi. Feri huvukisha takriban abiria mia tatu na takriban magari 6,000 kila siku. Naibu Spika wa Muda, ukweli ni kwamba chombo hiki kinatembea baharini lakini aibu ambayo hivi sasa imeonekana ni kwamba kwenye feri hakuna watu wenye uzoefu na uwezo wa kusaidia wakati ajali inapotokea. Haiwezekani kamwe chombo kama hiki kiwe kinafanya shughuli zake bila ya kuwepo kwa waokoaji wakati dharura inapotokea ilhali chombo kile kinahudumia watu kwenye bahari. Mbali na Kenya Navy inavozungumziwa, haya ni madharau na kutowajibika; nikutojali na kutoheshimu wananchi wa Kenya. Serikali ya Kenya yapaswa kuwajibika kwa haya yote. Hii ni kwa sababu wananchi wanalipa kodi kuhakikisha kwamba wanapata huduma. Leo ni siku ya tatu na Serikali nzima imeshindwa kuliokoa lile gari na maiti. Ikiwa tutazungumza hivi kwa ajali ya mtu mmoja, ingekuwa na watu wengi je? Vilevile, mara nyingi twahisi kwamba haya ni madharau kwa upande wa Serikali. Ingekuwa ni mgeni kutoka Uingereza ama sehemu nyingine ya ulimwengu, pengine usiku ule ule kungefanywa kazi na shuhuli hiyo kukamilishwa. Ninaiomba Kamati husika ihakikishe kwamba wamelifuatilia suala hili kikamilifu na kuleta Mswada ama pendekezo kwamba haitakuwa sawa kwa KFS kutoajiri vijana ambao ni wapiga mbizi mahodari na wenye uzoefu mkubwa baharini. Tunao vijana hao Pwani."
}