GET /api/v0.1/hansard/entries/950019/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 950019,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/950019/?format=api",
"text_counter": 186,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Asante sana, Bi Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii ili kuunga mkono Mswada huu. Kwanza, ninataka kushukuru mheshimiwa kwa sababu Mswada huu unapendekeza kuwa sehemu fulani zitatengewa wachuuzi rejareja wafanyie biashara zao. Pili, Mswada huu unapendekeza kwamba sehemu ambayo itatengewa wachuuzi rejareja inapaswa kuwa na vyoo vya kutumia na usalama. Hii ni kwa sababu inavunja moyo kwa mtu yeyote kuambiwa afanye kazi mahali ambapo hakuna usalama na vyoo vya kutumia. Jambo lingine ni kwamba ukitembea katika sehemu nyingi huku Kenya, utaona kwamba wachuuzi rejareja wanaishi maisha ya kukimbizwa kila wakati; wanaishi maisha kama ya swara. Unapata kwamba askari wa kaunti ambao wameajiriwa, ni watu wa miraba minne na kazi yao ni kuwafurusha wachuuzi na kuwanyang’anya au kupora mali yao na kuwachapa. Kwa hivyo, kwa Mswada huu utakuwa wa manufaa sana kwa wananchi wa Kenya. Mswada huu unapendekeza kwamba ikiwa kaunti inataka kuwatimua wachuuzi ambao wamekubaliwa kufanya biashara katika mahali fulani, lazima wapatiwe notisi ya siku 30. Hilo ni jambo muhimu sana kwa sababu ataweza kujipanga na kujua kwamba ikiwa ataondoshwa mahali hapo, basi atapelekwa mahali pengine. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}