GET /api/v0.1/hansard/entries/950020/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 950020,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/950020/?format=api",
"text_counter": 187,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Seneta wa Kakamega amesema kwamba sisi hatuna haja ya kuujadili Mswada huu. Nataka kumkosoa kwamba sisi tuko na haki ya kuujadili Mswada huu, kwa sababu tuna jukumu la kuwaangalia wachuuzi wa reja katika kaunti zetu kwa sababu ugatuzi umekuja. Hizo ni sehemu ambazo tutaziangalia. Kwa hivyo, naiomba Kamati inayohusika iaangalie zile sehemu zinazosema kwamba Waziri wa Serikali Kuu ndiye atakayehusika. Tuko na mawaziri wetu katika kaunti zetu, na watayaangalia mambo haya kwa marefu na mapana. Ni vizuri ijulikane wazi kwamba sisi, kama Seneti, tunapaswa kuangalia mambo haya ndio tuweze kuwa na usawa katika nchi yetu ya Kenya, na katika kaunti zetu zote 47. Kwa hivyo, nasimama kuunga mkono Mswada huu. Wakati Kamati hiyo itakapoangalia Mswada huu, basi waangalie mambo ya kodi. Hawa ni wafanyabiashara reja reja, na hatuwezi kuwalinganisha na watu ambao wako na maduka makubwa ama wafanyabiashara waliobobea tayari katika biashara zao. Hawa ni watu wanaojaribu kujiinua katika maisha yao. Kwa hivyo, tunaomba watozwe kodi kulingana na biashara zao. Hii ni kwa sababu ukiwatosha kodi kubwa, hatutakuwa tukiwasaidia Wakenya, ila kuwafukuza katika biashara. Tungependa tuwape motisha ili walipe ushuru. Jambo lingine ni kuwa kwa sababu wao ndio wanaolipa ushuru mkubwa katika nchi yetu, basi tunapaswa tuwapatie stima pale mahali wanapofanyia kazi ili waweze kufanya kazi kutoka asubuhi mpaka jioni."
}