GET /api/v0.1/hansard/entries/950045/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 950045,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/950045/?format=api",
    "text_counter": 212,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante Bw. Spika wa Muda kunipa fursa hii ili kuwasilisha Hoja ya kuairishwa kwa Bunge ili tuweze kujadili kuhusu ajali iliyotokea katika kivuko cha feri cha Likoni, Mombasa County, mnamo Jumapili, 29th September, 2019. Vile vile, tunafaa kujadili hali ya huduma katika kivuko cha feri cha Likoni. Bw. Spika wa Muda, nasimama hapa leo kwa masikitiko makubwa kuzungumzia swala la ajali hiyo ambayo ilitokea katika kituo cha feri cha Likoni. Mnamo 29th September, 2019, mwendo wa 6:10 p.m., Mariam Kigenda na binti yake Amanda Mutheu waliabiri feri kwa jina MV Harambee kuvuka kutoka upande wa Likoni kwenda mjini. Feri ilipofika katikati ya bahari, gari lilirudi nyuma na kutumbukia baharini. Habari zilizoko ni kwamba ajali hiyo ilitokea kwa sababu gari lilirudi nyuma. Kulingana na kanuni, magari yanayoingia kwenye feri yanafaa kuzimwa . Hakuna jinsi dereva wa gari anaweza kurejesha gari nyuma baada ya kuingia kwenye feri . Baada ya ajali hiyo kutokea, jambo la kusikitisha ni kwamba, hakuna usaidizi wowote ulitolewa wakati ule. Baadhi ya wananchi waliokuwa pale walichukua video na picha zinazoonyesha gari lilivyozama pole pole mpaka likatumbukia kabisa ndani ya maji. Jambo la kusikitisha pia ni kwamba, hakuna aina yoyote ya huduma za dharura katika kivuko cha feri cha Likoni. Kwa mfano, hakuna ambulansi, mashua na waogeleaji wa kuokoa. Kukitokea dharura, wananchi hawawezi kusaidika mara moja ili kupunguza maafa. Ikumbukwe kwamba, mnamo 1994, Feri ya Mtongwe kwa jina Mv Mtongwe ilizama katika kivuko cha feri cha Mtongwe. Ilikuwa kama mita 10 hivi kutoka makao makuu ya Jeshi la Wanamaji la Kenya. Watu 250 walifariki kutokana na mkasa huo. Inajulikana wazi kwamba tayari maafa yalishatokea na kwa hivyo, wakati wowote maafa yanaweza kutokea. Ni jambo la kusiskitisha kwamba, Kenya kupitia shirika la Kenya Ports Authority (KPA ) ilitia sahihi mkataba wa International Maritime Organization (IMO) ambao unatoa kanuni fulani kuhusiana na maswala ya usalama ya vyombo vya bahari. Kwa hivyo, The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}