GET /api/v0.1/hansard/entries/950046/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 950046,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/950046/?format=api",
"text_counter": 213,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "usalama wa Bandari ya Mombasa pamoja na kivuko cha feri cha Likoni umo mikononi mwa Harbour Master ambaye ndiye mkuu wa usalama katika Bandari ya Mombasa. Ni jambo la kusikitisha kwamba, Bandari ya Mombasa haina vifaa vya kutosha vya kuweza kupambana na majanga kama hayo. Bw. Spika wa Muda, lawama inaelekezwa kwa shirika la Kenya Ferry Services (KFS), Wizara ya Usafiri na Miundomsingi, Shirika la KPA, Kenya Coast Guard Services ambayo ilizinduliwa juzi na vilevile Kenya Maritime Authority (KMA) . Shirika la KMA lina jukumu la kuhakikisha kwamba vyombo wanavyoabiri binadamu katika bahari za Kenya viko katika hali nzuri na vina insurance na kuna vifaa vya dharura ambavyo vinaweza kutumika kuhakikisha kwamba wananchi hawapati maafa kukitokea dharura. Kaunti ya Mombasa imekuwa ikipigania kuhusishwa kwa usimamizi wa huduma za feri lakini Serikali imekataa. Ikumbukwe kwamba, kabla ya Shirika la Kenya Ferry Services, huduma za feri zilikuwa zinasimamiwa na Baraza la Mji wa Mombasa pamoja na kampuni ya kibinafsi ya Kenya Bus Service (KBS) . Shirika la Kenya Ferry Services liliundwa baada ya kuanguka kwa KBS. Wakati huo, Shirika la KPA lilikuwa na asilimia kubwa ya rasilmali na likawa linafanya kazi katika kivuko kile. Kwa hivyo, si jambo la ajabu Kaunti ya Mombasa kupewa usimamizi wa huduma za feri kwa sababu ni jambo ambalo tayari watu wa Mombasa walikuwa wanafanya. Ni kama mtu kurudi nyumbani kwao alikozaliwa baada ya kutoweka kwa muda mrefu. Ukizingatia uwekezaji katika huduma za feri, ni wazi kwamba Serikali haijatilia maanani dharura ya kuhakikisha kwamba vivuko vya feri ni salama. Kwa mfano, FY 2007/2008, Serikali ilitoa karibu Kshs956 milioni kusimamia mambo ya mishahara ya wafanyakazi katika vituo vya feri na vile vile kununua vifaa. Katika FY 2018/2019, Serikali ilitenga Kshs293 miloni . Kinaya ni kwamba FY 2019/2020, pesa ambazo zimetengwa ni Kshs235 milionI pekee. Hii inamaanisha kwamba Serikali imepunguza pesa hizo. Kuna changamoto nyingi katika vituo vya feri. Kwa hivyo, upunguzaji wa fedha umekuwa ukiathiri pakubwa huduma zinazotolewa katika vituo vya feri. Ikumbukwe kwamba, wananchi hawalipi wanapotumia feri kuvuka. Ni magari pekee yanayolipishwa. Tunapozungumzia swala hili, kwanza kabisa tunafaa kujiuliza kwa nini shirika la Kenya Ferry Services halina vifaa vya kisasa vya usalama katika sehemu zile. Jambo la pili ni kwamba, kati ya feri tano ambazo zinafanya kazi, ni feri moja pekee ambayo ina milango ambayo inaweza kufungwa magari yakishaingia na kufunguliwa wakati yanapotoka. Milango ya feri nne haiwezi kufungwa. Kwa hivyo, binadamu, gari, ama chombo chochote kinaweza kuanguka wakati wowote. Kwa nini hawakuweka vifaa vya usalama kama vile vizuizi kuhakikisha kwamba magari yaliyopandishwa pale juu na binadamu wako salama? Kwa nini hatujanunua vifaa vya kisasa vya usalama kama vile speed boats ambazo zinaweza kutumika wakati kuna dharura; vifaa vya kuingia ndani ya bahari na vinginevyo? Kwa nini Shirika la Huduma za Feri halijaajiri wazamiaji wenye tajiriba kuu ya ujuzi kama huo ili kuhakikisha kwamba kukitokea dharura wanaweza kuokoa maisha ya wananchi? The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}