GET /api/v0.1/hansard/entries/950047/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 950047,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/950047/?format=api",
    "text_counter": 214,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Mwisho ni kwa Jeshi la Wanamaji, Kenya Ports Authority (KPA) na Kenya Maritime Authority (KMA); wana mipango gani kuhusiana na usalama katika kivuko cha Likoni na Bandari kwa jumla? Tangu juzi hadi sasa, gari lao na wale waathiriwa hawajapatikana. Wameweka mikakati gani kuhakikisha kwamba iwapo kutatokea tukio kama hili wakati mwingine, uwezekano wa kuokoa maisha na mali utakuwa mzuri zaidi kuliko ilivyofanyika juzi? Mtakumbuka ya kwamba, tushawahi kupoteza maisha ya watu takriban 200 katika kivuko cha Mtongwe ambacho kinahudumia watu wengi."
}