GET /api/v0.1/hansard/entries/950048/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 950048,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/950048/?format=api",
"text_counter": 215,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Tangu Shirika la Huduma za Feri kuundwa, ijapokuwa limetajwa kwamba ni Shirika la Kitaifa, mpaka sasa hawajaweza kutoka nje ya Kaunti ya Mombasa kufanya huduma yoyote. Hatujaweza kununua feri ambazo zinaweza kuhudumu katika Ziwa Victoria, Ziwa Turkana na kwengineko ambako kuna usafiri wa majini. Ni swala ambalo Kaunti ya Mombasa inaweza kusimamia kikamilifu kwa sababu ruzuku inayotolewa na Serikali imepungua pakubwa. Kwa vile imepungua, inamaanisha kwamba huduma katika eneo hilo zitaathirika na wananchi watakosa huduma bora. Hatuombi iwe hivyo, lakini kukitokea dharura nyingine, itakuwa shida kwa wananchi kuweza kupata huduma bora ili kuokoa maisha."
}