GET /api/v0.1/hansard/entries/950080/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 950080,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/950080/?format=api",
"text_counter": 247,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Nampongeza Seneta wa Mombasa kwa kuleta Hoja hii. Ni jambo la kushangaza kwamba jambo hili lilipotendeka tukiangalia katika zile picha ambazo zilipigwa na kusambazwa zinaonyeshana kwamba kulikuwa na muda wa dakika kadhaa kabla ya gari kuzama kabisa. Najiuliza kama pale hapakuwa na wapiga mbizi ambao wangewaokoa mama na mtoto walipokuwa wakizama. Pili, tunaambiwa kwamba katika sehemu ile kuna wanajeshi wetu ambao wanalinda mipaka baharini. Walifanya nini?"
}