GET /api/v0.1/hansard/entries/950083/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 950083,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/950083/?format=api",
"text_counter": 250,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Spika wa Muda, hii sio mara ya kwanza jambo kama hili kutokea. Tumekuwa na feri ambayo ilizama pale lakini hakuna hatua ambayo ilichukuliwa ili janga kama hili lisionekane tena. Ni kana kwamba jambo likitendeka tunaongea halafu inakuwa hayo mambo yanasahaulika na maisha yanaendelea kama kawaida. Jambo likitendeka linatakiwa liwe ni funzo kwetu ili tuweze kujikinga nalo siku za usoni. Inaonekana kwamba sisi tunaongea halafu tunakwenda zetu. Serikali inapaswa ichukue jambo hili kwa makini sana. Kama vile Seneta alivyosema, pesa ambazo hutengewa idara hii hupunguzwa kila uchao. Maafa hayo yanapotokea idara hii haina pesa za kutosha kudhibiti na kujikimu. Maafa kama haya yanapotendeka, inakuwa jambo ambalo haliwezi kuzuiwa."
}