GET /api/v0.1/hansard/entries/950093/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 950093,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/950093/?format=api",
"text_counter": 260,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13224,
"legal_name": "Golich Juma Wario",
"slug": "golich-juma-wario"
},
"content": "Asante Bw. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii. Nitatangulia kwa kutuma risala za rambirambi kwa familia ya marehemu mama Mariam, jamaa na marafiki. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Seneta wa Mombasa amefanya vizuri kuleta Hoja hii kwa sababu wengi wamekufia ndani ya maji na wengi wako katika hatari ya kutumbukia majini. Utashangaa ukiingia katika feri ya Likoni kwa sababu magari na watu wanaingia kwa wingi. Hakuna mlango wa kufungwa baada ya watu kuingia. Kwa hivyo, hakuna chochote cha kuzuia watu na magari kuanguka ndani ya maji."
}