GET /api/v0.1/hansard/entries/950094/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 950094,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/950094/?format=api",
"text_counter": 261,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13224,
"legal_name": "Golich Juma Wario",
"slug": "golich-juma-wario"
},
"content": "Siku zote, mimi hujiuliza maswali. Sijui feri hutengenezwa namna gani. Ukienda pale, utaona kuwa magari na watu huingia kwa wingi lakini mlango haufungwi. Endapo gari litakosa mwendo, hakuna chochote cha kulizuia kutumbukia majini. Katika karne tunayoishi sasa, kuna vifaa vingi vya kisasa vya kuzuia maafa. Vile vile, kama walivyosema wenzangu, kuna watu ambao wamesomea mambo ya maji. Kuna wapigambizi ambao wanaweza kuzama ndani ya maji na kuangalia kilichoko majini na kukitoa. Pia, kuna maafisa wa Jeshi la Wanamaji ambao wanafunzwa mambo ya maji na wanaweza kunusuru kitu kikianguka majini. Tangu gari hilo lilipotumbukia majini, wapigambizi wamejaribu kulinusuru lakini wameshindwa. Inasemekana kuwa gari hilo lilining’inia juu ya maji kwa muda mrefu. Msaada mkubwa ulikuwa watu kuchukua video na picha na kuliangalia tu likizama polepole. Hii inamaanisha kuwa kuna watu ambao wamezembea katika kazi zao. Katika karne hii, watu hawafai kuzembea kazini na kusababisha watu maskini kuanguka na kuzama majini. Waliokufa, Mungu awapeleke pema. Kuna hatari kubwa sana kwa sababu watu huvuka kwa maelfu kutoka South Coast kwenda Mji wa Mombasa kila wakati. Endapo hatua yoyote haitachukuliwa, basi wanaotumia huduma za feri watazidi kuwa katika hatari. Wakati mwingi mimi na Sen. Faki huenda katika Mji wa Mombasa na tunatumia feri kuvuka kutoka upande mmoja hadi mwingine. Sisi pia tuko hatarini."
}