GET /api/v0.1/hansard/entries/950103/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 950103,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/950103/?format=api",
"text_counter": 270,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Zani",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13119,
"legal_name": "Agnes Zani",
"slug": "agnes-zani"
},
"content": "Asante sana Bw. Spika wa Muda. Ningependa kumshukuru Sen. Faki kwa kuleta Hoja hii muhimu. Tangu janga hilo lilipotendeka, nchi nzima imeshtuka. Wengi wetu walishuhudia tukio hilo kupitia simu zetu za rununu. Mara kwa mara hatuna nafasi ya kushuhudia mtu akifa. Gari hilo lilielea juu ya maji kwa dakika kama ishiri hivi. Sitaki kufikiria mama yule na mtoto wake walikuwa wanafikira vipi wakati gari lao lilikuwa linaelea kwa maji. Nadhani walikuwa na imani mtu angewasaidia. Watu waliokuwa ndani ya ferry walipiga mayowe na kuomba. Wengine walijaribu kutafuta njia ya kuokoa waliokuwa kwenye gari ilipokuwa linaelea lakini wakakosa njia. Wapiga mbizi wawili walijaribu kuruka kwenye maji lakini hapakuwa na matayarisho yoyote kuhakikisha kwamba gari hili lingenusuriwa. Katika janga hili, gari lilizama majini. Je ingekuwa janga linguine kwa mfano; je meli ingegonga feri hilo au tukio lolote la dharura lingetokea? Watu wengi wanaotumia ferry, wanaamini kwamba kuna usalama. Kivukio cha feri ya Likoni kinatumika na watu wengi kutoka upande wa Kwale wakija upande wa Mombasa na kutoka upande wa Mombasa kuenda upande wa Kwale au hata kuenda mpaka Tanzania. Kuna watu hupita ferry kwa njia ya kufanya biashara kila siku. Pia kuna wale hupeleka watoto wao shuleni wakitumia ferry. Watu wengi sana hutumia ferry kila wakati. Tukio hilo limedhihirisha kwamba hakuna usalama katika ferry. Kenya Marine The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}