GET /api/v0.1/hansard/entries/950104/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 950104,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/950104/?format=api",
"text_counter": 271,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Zani",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13119,
"legal_name": "Agnes Zani",
"slug": "agnes-zani"
},
"content": "Authority na Kenya Coastal Guards ambao kazi yao ni kuhakisha kwamba kuna usalama majini wana ofisi zao karibu na pahali tukio hilo lilitokea lakini hawakusaidia. Tumekuwa tukizungumzia utovu wa usalama wa watu na magari ambayo hutumia ferry. Inamaanisha kwamba kuna jambo ambalo linabidi kufanywa lakini ikifika katika mambo ya usalama au kifo, tunaamini kwamba katika nyanja yoyote, lazima kuwe na wale waliojitayarisha kwamba jambo kama hili likitokea, wanaweza kujitokeza. Sen. Wetangula ametuhusisha juu ya waziri tofauti katika nchi ya India ambaye alijiuzulu wakati janga la gari la moshi lilipotea katika nchi yao. Waziri huyo alichukulia jambo hilo kuwa muhimu na kurekebisha. Mara kwa mara, huwa hatujitayarishi jinsi ya kurekebisha mambo yanapoenda kombo na jinsi ya kurekesbisha. Tukiangalia ajali ambayo inawezakutokea kama ile ambayo ilitokea kwa ferry, ni mambo kidogo kidogo ya hapa na pale ambayo yanafaa kuhakikishwa yamewekwa. Kwa mfano, kama magari yameingia kwa feri, yanafaa yahakikishwe yamezimwa. Kwa muda mrefu, Feri imekuwa na bamba ambalo linajitokeza kwa upande wa nyuma kuhakikisha kwamba mtu akiingia ndani, hawezi kurudi nyuma. Huyu mama, kwa sababu ambazo hazijajitokeza, aliingia kwenye feri na mtoto wake na watu wengine ambao alikuwa amewabeba na kwa bahati mbaya akaaingia ndani ya maji. Tulifikiria katika dakika ishirini angeweza kuokolewa, lakini, hakuweza kuokolewa. Hili ni jambo ambalo limeingiza hofu kwa sababu wale wanaovuka ferry wanafikiria vile watakavyofanya. Sen. Faki ameleta Hoja hii muhimu ili tuhakikishe njia ya kivukio cha feri ya Likoni kiko salama ili watu waweze kuvuka bila tashwishi au uoga kwamba wataingia kwenye feri. Mambo kama hayo huwa yanajitokeza lakini kama majanga ambayo yanajitokeza hayaangaliwi na kurekebishwa, yatarejelea. Kwa vile janga hili limetokea, ni muhimu turudi nyuma tuangalie ili lisitokee tena. Tunafaa tuangalie usalama wa wale wanaingia na kutoka kwenye feri umedhihirishwa. Kwa mfano, kuna hadithi tofauti tofauti ambazo watu wanasema za vile ambavyo mtu anaweza kujiokoa jambo kama hili likitokea. Lakini, juzi tuliona wapiga mbizi wakivuka na kujaribu kwenda upande ule mwingine wakati ambapo ferry haikupatikani. Juzi tena, tuliona ferry ikipita na meli pia ilikuwa inapita. Wale waliokuwa kwenye feri walipiga mayowe na makelele wakifikiria kwamba watagongana. Kwa hivyo, kuna tashwishi. Lazima jambo hili liwekwe kipaumbele kuangalia nini haswa chanzo cha ukosefu wa usalama katika feri. Tunafaa tuhakikishe kwamba tumetafuta mbinu au watu fulani ambao wataketi kuhakikisha jambo hili limesuluhishwa. Hebu fikiria watoto wadogo ambao walikuwa kwenye feri ambao waliona mambo haya yakifanyika? Yule ambaye amekufa na wale wadogo ambao waliona yote yakifanyika. Baadaye, kulikua na kikao cha watu kwenye feri wakilia, wakiomba na kufikiria wale ambao walikufa. Wakati mwingine kuna vile vizuizi vinaweza kuwekwa kwenye feri, kama vile kwa upande ambao watu wamesimama. Hii ni kwa sababu unaweza kuona mtu amepatwa na ugonjwa au kupoteza fahamu na kuanguka. Vizuizi vinafaa kuwekwa pale kuhakikisha kwamba mambo kama haya hayafanyiki. Zamani walikuwa wanaweka kitu kidogo cha kusimamia ili kuhakikisha watu hawatoki. Baada ya janga hili, ni muhimu kuangalia vile The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}