GET /api/v0.1/hansard/entries/950285/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 950285,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/950285/?format=api",
"text_counter": 176,
"type": "speech",
"speaker_name": "Wundanyi, WDM-K",
"speaker_title": "Hon. Danson Mwashako",
"speaker": {
"id": 13509,
"legal_name": "Danson Mwashako Mwakuwona",
"slug": "danson-mwashako-mwakuwona"
},
"content": " Mhe. Naibu Spika wa Muda, nashukuru kwa nafasi hii. Nasimama kuunga mkono Mswada huu ulioletwa na mwenzetu Mhe. Nyoro kuwa hukumu na faini inayotolewa kwa wafisadi ipate kuongezeka maradufu. Kila mara tunapokaa katika Bunge hili na kuongea juu ya masuala ya ufisadi, nafikiri nchi nzima huwa inatuangazia sana kama viongozi. Ni jambo la kusikitisha sana kuwa nchi hii ambayo inajulikana katika Afrika na ulimwengu mzima kuwa ni nchi ambayo inastawi, tunajulikana kwa masuala ya ufisadi. Tumewekwa katika jedwali katika nchi za Afrika na inaonekana kuwa Kenya imestawi sana na mambo ya ufisadi. Leo hii wanariadha wetu kule Doha wanaleta sifa nyingi kwa nchi yetu. Lakini vilevile, mara nyingine wakati tunapeleka wanariadha kule kushindana duniani bado masuala ya ufisadi yanaingia ndani. Tunakumbuka yale yaliyotendeka miaka miwili au mitatu iliyopita, wakati tulipeleka timu ya nchi lakini ufisadi ukaingia sana. Leo Wakenya wanalia. Wengi wao wako katika hali ya umaskini kwa sababu wale waliopewa nyadhifa za uongozi miaka ya mbele, wengine hata walipewa urais, kila mmoja kutoka juu mpaka chini kwa yule askari anayechunga mlango wa hospitali, wanajitafutia mafanikio kupitia njia ya ufisadi. Rais alitangaza vita vikali sana dhidi ya ufisadi. Aliwapa nyadhifa za kazi Mawaziri na tukadhani kwamba kipindi hiki tutaona kweli watu wakihukumiwa. Tulidhani kwamba tutaona watu wakipigwa faini kubwa ili Wakenya wazidi kuwa na imani kuwa ufisadi kweli tunapigana nao. Nadhani kuwa Bunge hili sasa limepata nafasi ya kutoa maoni yake kwa uzito kabisa. Maoni yetu tutatoa kivipi? Kupitia sheria kama hii. Sheria hii ni nzuri. Lazima sauti yetu ya kupigana na ufisadi izidi kuenda juu. Itaenda juu wakati tunasema kwamba ukiiba pesa ya umma… Hesabu inafanywa na Mkaguzi wa Vitabu Vya Serikali na inakuja katika kamati yetu ya masuala ya pesa na tunajadili. Tunajua kwamba kwa kaunti fulani, gavana fulani, eneo Bunge fulani au wizara fulani pesa zimepotea lakini hakuna atakayepelekwa mahakamani."
}