GET /api/v0.1/hansard/entries/950286/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 950286,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/950286/?format=api",
"text_counter": 177,
"type": "speech",
"speaker_name": "Wundanyi, WDM-K",
"speaker_title": "Hon. Danson Mwashako",
"speaker": {
"id": 13509,
"legal_name": "Danson Mwashako Mwakuwona",
"slug": "danson-mwashako-mwakuwona"
},
"content": "Wakati Mkaguzi wa Vitabu vya Serikali amesema pesa fulani imepotea katika eneo Bunge langu ama katika ofisi fulani ya Serikali, wacha yule atakayepatikana na makosa yale arudishe ile pesa mara mbili inavyoandikwa katika sheria hii. Tukifanya hivyo, huenda tukapunguza tamaa ambayo watu wengi wanaopata nafasi za Serikali wako nayo. Ni vibaya sana kwamba wale wanaolala korokoroni, wale waliohukumiwa, wengi ni kwa makosa madogo madogo ambayo yanadhuru mtu mmoja ama wawili. Lakini makosa makubwa hufanyika wakati watu wanakufa mahospitalini, kwa mfano, katika Hospitali Kuu ya Kenyatta. Watu wanakufa hospitalini lakini wale waliopora pesa ya madawa wanapopelekwa kortini, mara nyingi kesi haina ushahidi ama hata ikiwa na ushahidi, wale wanaohukumiwa ni watu wa chini tu kuliko The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}