GET /api/v0.1/hansard/entries/950288/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 950288,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/950288/?format=api",
"text_counter": 179,
"type": "speech",
"speaker_name": "Wundanyi, WDM-K",
"speaker_title": "Hon. Danson Mwashako",
"speaker": {
"id": 13509,
"legal_name": "Danson Mwashako Mwakuwona",
"slug": "danson-mwashako-mwakuwona"
},
"content": "Kwa hivyo, wakati tunapojadili suala hili kama Waheshimiwa, ni vizuri itoke wazi. Hata kama nakubaliana na Mheshimiwa aliyesema kuwa tupatie mahakama uhuru wa kuamua ni vipi, kesi iko namna gani, hili ni jambo zuri katika sheria. Lakini mahali nchi hii imefika, tunajua ufisadi unatendeka hata ndani ya mahakama. Kwa hivyo, tukizidi kupatia wahukumu wetu uhuru wa kuamua ni nani atafungwa miaka kumi au mmoja, bado ufisadi utaingia maeneo yale. Ndiposa nakubaliana na Hoja hii kwamba tuwache mambo ya ufisadi… Maanake hata kwa mahakama upo. Wacha tutoe huo uamuzi kama Bunge, na tuseme kuwa ukipatikana umeiba pesa za umma, utarudisha mara mbili na ufungwe miaka isiopungua kumi kwa sababu vizazi vinavyokua vitatuhukumu vibaya sana kwa maana hawatapata kitu katika nchi hii."
}