GET /api/v0.1/hansard/entries/950303/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 950303,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/950303/?format=api",
"text_counter": 194,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu CWR, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
"speaker": {
"id": 786,
"legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
"slug": "ruweida-mohamed-obo"
},
"content": "Huko Lamu tatizo kubwa ni mihadarati kwa sababu ufisadi ndio unachangia pakubwa. Ukiangalia roadblocks kutoka Malindi mpaka Lamu ni zaidi ya kumi. Pia kuna zingine nyingi lakini mihadarati hupita na watoto wanatumia. Hii yote imesababishwa na ufisadi. Ardhi pia iko na changamoto sana lakini ni matumaini yetu kwamba, tume tuliyochagua itafanya kazi nzuri. Tamaa ikizidi ndiyo inaleta haya matatizo. Hivi sasa, huko Lamu kunapimwa na utasikia watu wametoka kaunti zingine ili wapatiwe ardhi. Ile ardhi ya Lamu iko na wenyewe. Kabila zote zilizoko Lamu zina haki kwa sababu ni ardhi yao. Lakini wanaotiririka kutoka kaunti zote hadi Lamu wajue Kaunti yetu ya Lamu ina wenyewe. Hiyo itachangia ufisadi na hatutakubali. Kuhusu elimu, kila nikizugumza sitakosa kuitaja wadi ya Basuba. Hii pia imeguzwa na ufisadi. Shule ilipoporomoka Dagoretti, Serikali yote ilienda hapo. Lakini Lamu mpaka sasa miaka mitano imepita na shule za Basuba Wadi zimefungwa na hatujaona Serikali ikishuka na kusema huko ni muhimu. Waziri ameenda huko na kuona zimefungwa. Nani ataamini kama hapa Kenya kuna shule ambayo miaka mitano imepita na bado haijafunguliwa? Sio kwamba hatufanyi bidii. Nimeuliza Swali hapa Bungeni na saa hii ninaandika petition . Ufisadi ukiangaliwa vizuri, elimu itakuwa nzuri Kenya nzima. Tukizungumza mambo ya Likoni Ferry na matatizo yanaonekana, dunia nzima imeona udhaifu wetu. Tatizo hili pia linasababishwa na ufisadi. Kwa mfano, huko Kizingitini, kuna vijana hodari wa kuzamia baharini lakini hawachukuliwi. Sisi tunajua mahodari ni akina nani lakini wataulizwa stakabathi na hawana. Kuna vijana kama Captain Bady. Ikitokea tatizo, mimi nawapongeza sana watu wa Lamu kwa sababu sisi hatungoji wengine. Mambo mengi yametokea na wao wenyewe wanazamia hawaogopi wanaenda kusaidia. Lakini vibali ndivyo hawana. Athuman Bady anajulikana. Ukitaja divers, kunajulikana Kizingitini kuna divers wazuri lakini The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}