GET /api/v0.1/hansard/entries/950383/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 950383,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/950383/?format=api",
"text_counter": 274,
"type": "speech",
"speaker_name": "Taita Taveta CWR, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Haika Mizighi",
"speaker": {
"id": 13274,
"legal_name": "Lydia Haika Mnene Mizighi",
"slug": "lydia-haika-mnene-mizighi"
},
"content": "kwa sababu ya suala hili la ufisadi. Mahospitali hayana madawa na watu wanakufa ovyo ovyo. Ukifuatilia sana, unapata ni kwa sababu ya ufisadi. Kuna kisa kimoja cha ufisadi kilichonishangaza sana. Kilinisababisha kutambua ufisadi umefanya watu kupenda mali zaidi, hata utu umewatoka. Dereva wa ambulance alienda kuchukua mgonjwa ambaye alikua ni mama mja mzito aliyekuwa karibu kujifungua. Lakini kufika pale, akasema kwanza anataka afungiwe kitu chake kidogo ambacho hakina risiti wala hakijulikani mahali popote akiweke mfukoni ndiposa waende. Ni huzuni kwa maana tulimpoteza huyo mama. Nilimshughulikia yule dereva vilivyo kwa sababu nilivyofahamishwa hali hiyo sikufurahi. Hiki ni mojawapo ya visa vya ufisadi nchini. Visa kama hivi vinawafanya sisi viongozi kudharauliwa. Tazama kisa kilichotokea pale Likoni Ferry, Mombasa. Ni siku tatu sasa na hali haieleweki. Kumekuwa na mauti pale na mpaka sasa watu wanakaa katika hali wasiyoifahamu. Kuna utepetevu ambao haueleweki. Tukiangalia kwa mtazamo, tunaona ni kwamba kuna ufisadi ambao unaendelea pale. Kenya nzima hakuna watu wa kuokoa hali kama hiyo? Mhe. Naibu Spika wa Muda, ndio maana ninaunga mkono suala hili kwamba kuwe na hukumu kali kwa mambo ya ufisadi."
}