GET /api/v0.1/hansard/entries/950394/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 950394,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/950394/?format=api",
"text_counter": 285,
"type": "speech",
"speaker_name": "Taita Taveta CWR, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Haika Mizighi",
"speaker": {
"id": 13274,
"legal_name": "Lydia Haika Mnene Mizighi",
"slug": "lydia-haika-mnene-mizighi"
},
"content": " Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nilikuwa ninasema kwamba tumeona watu wengi ambao wamehusishwa na masuala ya ufisadi katika nchi hii ya Kenya lakini kufikia sasa, ni kama hatua inayofaa kuchukuliwa haijachukuliwa kwa sababu wengi wao wako huru. Wengi wao ni majina tajika na viongozi ambao tunaweza kuwaita kwa kiingereza role models . Hii inasababisha hali hii ya ufisadi kuonekana kama ni hali ya kawaida. Hakuna hofu kabisa ya mtu kutotaka kufanya ufisadi wa hali yoyote kwa sababu wale ambao wamehusishwa wako huru na wanaendelea kuishi maisha yao ya kawaida. Basi watu wanaona kwamba ufisadi umekuwa ni jambo la kawaida."
}