GET /api/v0.1/hansard/entries/951313/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 951313,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/951313/?format=api",
    "text_counter": 270,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
    "speaker": {
        "id": 786,
        "legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
        "slug": "ruweida-mohamed-obo"
    },
    "content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii nami niuchangie Mswada huu. Elimu ni sekta muhimu sana. Nimekuwa hapa tangu saa nane na nusu nikingoja nami nipate nafasi nichangie. Nimekuwa na dharura muhimu; dadangu yuko hospitali katika chumba cha upasuaji lakini nimesema acha nikae hapa nami nipate hii nafasi. Hii ni kuonyesha umuhimu niliokuwa nao wa kuchangia Mswada huu. Ripoti nyingi za Kamati ya Elimu zikiletwa huzungumzia mambo mazuri sana. Kamati ya Elimu na Utafiti huleta ripoti nyingi ambazo zinazungumzia mambo mazuri sana na mikakati mingi ya kuboresha elimu. Nimeipitia Ripoti hii na ina mambo mengi muhimu ya kuboresha elimu. Mwanzo, wanazungumzia majukumu ya Serikali, elimu kama haki ya kibinadamu na upanuzi wa nyanja mbalimbali katika elimu. Ninaunga mkono lakini kama nimeketi hapa, naona tunapitishia Wakenya wengine. Inaonekana kuna Wakenya bora zaidi wakuwekea hii mipango."
}