GET /api/v0.1/hansard/entries/951318/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 951318,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/951318/?format=api",
    "text_counter": 275,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
    "speaker": {
        "id": 786,
        "legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
        "slug": "ruweida-mohamed-obo"
    },
    "content": "Hata mbinu za kisasa kama televisheni ama tarakilishi zingetumiwa ndio mtu akiwa Nairobi asomesha wale watoto. Jamii ndogo ya marginalised community iliyotengwa ya Basuba, Boni ana Aweer mpaka sasa hawana shule ya chekechea. Kila wakati nikienda kwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknologia, nasukumwa kwa Wizara ya Usalama. Nimetafuta suluhisho na sipati. Simwoni mwenyeketi wa kamati lakini anajua shida zangu. Nimeng’ang’ana lakini sipati suluhisho. Sijui wamelengea nini hawa watoto maanake Katiba inasema lazima wapatiwe haki zao. Mimi nasikia uchungu nikiketi hapa kupitisha Mswada mzuri uende kwingine lakini kwetu haufiki."
}