GET /api/v0.1/hansard/entries/952713/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 952713,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/952713/?format=api",
    "text_counter": 146,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Nataka kujumuika na wenzangu kutuma risala zangu na za watu wa Laikipia za rambirambi kwa jamaa ambao walipoteza watoto wao pale shuleni. Hili ni jambo la kuvunja moyo sana kwa kuwa katika Wizara yetu ya Elimu, kuna kile kitengo cha ukaguzi ambacho kinapaswa kuwa kimepitia pale kukagua shule vile ilivyo. Lakini inaonekaka hakuna chochote walichokuwa wamefanya. Hii ni kwa sababu darasa lilibomoka, watoto wengine wakapata majeruhi na wengine wakapoteza maisha yao. Bw. Spika, jambo linalovunja moyo sana ni kwamba hakuna hatua yoyote iliyo chukuliwa dhidi ya yule mwekezaji. Yeye anaonekana ni mtu mlafi na nilipomuona, alikuwa anatabasamu ni kama hakuna jambo lolote baya lililotendeka. Kwa hivyo, jambo la kwanza ambalo Serikali inapaswa kufanya ni kumchukulia mtu kama yule hatua kali ili iwe funzo kwa wawekezaji wingine wowote ambao kazi yao ni kutaka kuekeza na kutumia nguvu zao za hela ili kuwapotosha Wakenya na kuwaweka katika hali hatari ya maisha yao. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}