GET /api/v0.1/hansard/entries/952715/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 952715,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/952715/?format=api",
    "text_counter": 148,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika. Kwanza, kuna tabia inayoitwa utovu wa nidhamu, kwa sababu ya hawa mabepari wa ufisadi, haswa tamaa ya pesa iliyoingia zaidi katika huyu mwekezaji ama mwenye jengo hili. Hili ni jambo la kusikitisha kuliona likitendeka nchini Kenya, kwa sababu yeye alithamini pesa kuliko maisha ya watoto wetu tunaompelekea ili waweze kujifundisha kusoma, kupita mitihani na kuendelea. Hivi sasa, imekuwa tunampelekea watoto ili waweze kufa ndani ya madarasa. Hili ni jambo la kukemea zaidi. Bw. Spika, vile vile, ni muhimu Serikali ichukue hatua dhidi ya mwenye kumiliki shule hiyo; wale watu waliojenga, walioidhinisha ujenzi wa shule kama hiyo na kusema kwamba iko sawa, na watu wanaweza kuingia katika hayo madarasa ili wanafunzi waweze kusoma. Kisheria, tutaona kwamba yule aliye na nyumba ama yule mwenye shule ndiye atakayechukua jukumu la hatari yeyote itakayotokea pale kwa maisha ya wanadamu."
}