GET /api/v0.1/hansard/entries/952718/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 952718,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/952718/?format=api",
    "text_counter": 151,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Kwa hivyo, tunasema kwamba watoto wetu ni muhimu katika nyumba zetu na katika maendeleo ya Taifa letu la Kenya. Kwa hivyo, ikiwa watoto wetu wataaachiliwa kiholela, itakuwa ni jambo la kusikitisha iwapo shule kama hizi zitaendelea kujengwa kila mahali katika nchi yetu. Hii inahatarisha maisha ya watoto wetu. Kwa hivyo, nikiunga mkono, inafaa hatua ichukuliwe ya kupitisha mjengo ambao utaruhusiwa, ili watoto wetu waweze kuketi ndani ya madarasa tukijuwa kwamba wako salama salmin na wanaweze kusoma ili wawe viongozi wa siku za usoni. Asante."
}