GET /api/v0.1/hansard/entries/953066/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 953066,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/953066/?format=api",
"text_counter": 96,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu CWR, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
"speaker": {
"id": 786,
"legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
"slug": "ruweida-mohamed-obo"
},
"content": "Hili ni jambo la maana sana. Kama alivyosema Mheshimiwa Jaldesa, ni mama pekee anayeweza kufikiria jambo kama hili. Lakini pia ninawashukuru wale Waheshimiwa wanaume ambao wameunga mkono kwa sababu wameusikia ule uchungu wa mama. Kunahitajika muda wa kukaa na mtoto anapojikuta kwenye mazingira mapya. Kuna mambo mengi ambayo yule mama anahitaji kumuhudumia yule mtoto vizuri. Anastahili atafute shule nzuri na amkaribishe nyumbani. Kuna mambo chungu nzima yanayohitaji muda. Akipewa nafasi hiyo ataweza kuungana na yule mtoto vizuri. Kwa hiyo, ninaunga mkono hapo."
}