GET /api/v0.1/hansard/entries/953067/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 953067,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/953067/?format=api",
    "text_counter": 97,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
    "speaker": {
        "id": 786,
        "legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
        "slug": "ruweida-mohamed-obo"
    },
    "content": "Pili, ninaomba mashirika yanayohusika na jambo hili yawe yanafuatilizia kwa makini wahakikishe kwamba Watoto hao wameingia kwenye mikono mizuri yenye usalama. Nchi nyingine huchukulia masuala ya watoto kwa uzito mkubwa. Kwa mfano, kuna mtoto ambaye alizaliwa nje ya nchi, na amekuja Kenya. Tulishangaa kuona serikali ya kigeni ilimtuma afisa wa watoto kusafiri mpaka Chundwa, ambayo iko Lamu Kusini, kuja kuangalia kama yule mtoto yuko kwenye mazingira mazuri. Lakini, sisi Kenya hatufanyi jitihada zozote za kufuatiliza na kujua iwapo mtoto kama huyo yuko salama. Yule mtoto alikuwa ni wa Uingereza. Afisa wa watoto alitumwa kuja kuhakikisha kama mtoto yule anakaa vizuri huku Kenya au la. Kwa hivyo, ninaomba Serikali yetu pia ichukue majukumu kama hayo ihakikishe kwamba huyo mtoto yuko kwenye mazingira mazuri."
}