GET /api/v0.1/hansard/entries/953070/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 953070,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/953070/?format=api",
    "text_counter": 100,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
    "speaker": {
        "id": 786,
        "legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
        "slug": "ruweida-mohamed-obo"
    },
    "content": "Dadangu Mheshimiwa Jaldesa pia amegusia suala la madawa ya kulevya. Inafaa atoe mfano wa Lamu. Katika nchi hii, Lamu ndiyo imeathirika zaidi kutokana na utumizi wa madawa ya kulevya. Watoto wenye umri wa miaka 11 wanatumia madawa ya kulevya. Wanadanganywa. Mara nyingi hawajiingizi kwenye matumizi ya dawa za kulevya kwa hiari yao. Kuna maneno ambayo nikiyasema watu hapa wataniangalia mara mbilimbili. Hata hivyo, watu wengine huwadanganya watoto wanaojulikana kama lover boys; kwamba madawa hayo yatawasaidia kuongeza nguvu za kiumu ilhali ni uongo. Kwa hivyo, wanazitumia mwishowe wanajipata wako hapo bila kusaidika. Ni muhimu kuwachunga watoto wetu wote. Kuna changamoto nyingi ambazo bado hatujazishughulikia. Serikali ikitaka itaweza kuzifikia. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}