GET /api/v0.1/hansard/entries/953137/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 953137,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/953137/?format=api",
    "text_counter": 167,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Taita Taveta CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Haika Mizighi",
    "speaker": {
        "id": 13274,
        "legal_name": "Lydia Haika Mnene Mizighi",
        "slug": "lydia-haika-mnene-mizighi"
    },
    "content": " Ahsante, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii ili niweze kuchangia Mswada huu ambao ni mzuri. Ninampongeza Mhe. Martha kwa kuweza kuleta Mswada huu Bungeni. Kama akina mama, tunahusika sana kutetea masuala kama haya kwa sababu mara nyingisisi ndio hukaa na watoto na tunajua ni muda gani unahitajika kukaa nao ili waweze kuwekwa katika hali iliyo sawa. Ninaunga mkono Suala la kuweza kuwa na muda unaofaa na mtoto mdogo kwa sababu muda huu ndio utakaoruhusu kuweza kumjua mtoto vizuri naye akujue na utaweza kumfundisha maadili yanayofaa. Mara nyingi tunawakuza watoto bila ya kuwa na muda nao na wanakosa maadili na kuwa na tabia za ajabu ajabu. Utastaajabu ikiwa hiyo ni jamii yako uliyoweza kuikuza ama sivyo. Itatokea hivyo kwa sababa ya kukosa kuwa na muda unaofaa na jamii hiyo. Kwa hivyo, ninaliunga mkono suala hili. Muda unastahili uwe wa kutosha kati ya mtoto. Hata ikiwa ni baba, familia husika sharti iwe na muda wa kutosha na huyo mtoto wanaomchukua ili iweze kumpa maadili. Hivyo, watakuwa na wakati mzuri wa kujuana na kuelewana vizuri. Ahsante sana."
}