GET /api/v0.1/hansard/entries/953230/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 953230,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/953230/?format=api",
"text_counter": 260,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Hon. Ali Sharif",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Kwanza, ningependa kumpongeza Mheshimiwa kwa kuleta Hoja hii. Tunakubaliana sote kuwa ni Hoja muhimu sana na tunahitaji kuijadili kwa namna yake. Ukweli ni kwamba, mzazi yeyote anayepeleka mtoto shuleni huwa na malengo kwamba mtoto yule amalize shule na baadaye, awe kijana mwenye mwongozo katika ulimwengu wa leo. Lakini kwa masikitiko makubwa, suala hili limeonekana halina mwongozo na utaratibu. Sitaki niilaumu Serikali lakini nataka kuipa changamoto. Hii ni kwa sababu vijana wengi wanaomaliza shule wanapotea katika njia ambazo hazijulikani. Vijana wengi hawana kazi kwa sababu ya tatizo hilo. Kwa maana hiyo, kuna umuhimu mkubwa kuwe na mwongozo ambao utaambatana na Hoja hii. Mtoto yeyote anayemaliza shule ya upili sharti awe na uhakika, kupitia mwongozo wa Serikali kwamba, ataenda chuo kikuu ama chuo cha ufundi. Naipongeza Serikali kwa juhudi zake za kuweka mikakati kuhusu suala hili la vyuo vikuu na vyuo vya ufundi. Kuna dharura kubwa kuhakikisha kwamba mwongozo huu umefuatwa ili wanafunzi wanaomaliza shule wapate nafasi kujiunga na vyuo vya ufundi ama vyuo vikuu. Wengi wanaomaliza, hata wale wanaofaulu katika mitihani yao ya shule ya upili na wanahitajika kujiunga na vyuo vikuu, hukosa kufanya hivyo kwa sababu ya hali ngumu ya kiuchumi. Ingawa hivyo, kuna basari ambazo zinatolewa kufuatana na mwongozo wa Serikali. Litakuwa jambo la busara utaratibu huu ufahamike kwamba mtoto ambaye ataenda shule ya upili na amalize, sharti ajiunge na chuo kikuu ama chuo cha ufundi. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}