GET /api/v0.1/hansard/entries/953231/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 953231,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/953231/?format=api",
    "text_counter": 261,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ali Sharif",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": "Inasikitisha kuona kwamba wengi wa vijana wetu hawana mwongozo katika hali hii. Hawana kazi wala ujuzi na hawajasomea taaluma nyingine. Sio kwa sababu vijana hawataki kufanya hivyo, ni kwa sababu ya utaratibu na mpangilio wa Serikali yetu. Hiyo ndiyo inafanya vijana wakose imani katika jambo hili. Nikizungumzia Eneo Bunge la Lamu, hivi sasa, watu wengi wanafahamu kwamba tuko na Lamu Port-South Sudan-Ethiopia-Transport Corridor Project (LAPSSET). Lakini kwa masikitiko makubwa, jambo ambalo Serikali haijafanya ni kuhakikisha kwamba mradi huu umewasaidia vijana. Zile nafasi 1,000 ambazo ziliahidiwa na Serikali kwa vijana katika LAPSSET, hadi sasa, hazijawekwa bayana. Jambo hili halijafanyika. Kutokana na hilo, bado tunayo matatizo katika jamii. Kwa hayo machache, naunga mkono Hoja hii."
}