GET /api/v0.1/hansard/entries/953620/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 953620,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/953620/?format=api",
"text_counter": 369,
"type": "speech",
"speaker_name": "Wundanyi, WDM-K",
"speaker_title": "Hon. Danson Mwashako",
"speaker": {
"id": 13509,
"legal_name": "Danson Mwashako Mwakuwona",
"slug": "danson-mwashako-mwakuwona"
},
"content": "Pili, namshukuru Mhe. Sossion kwa kuleta suala hili Bungeni. Kenya nzima inaangalia vipi tutaangazia masuala ya usalama wa watoto wetu katika shule zetu. Ni jambo la majonzi na kusikitisha sana wakati watoto wetu wanapoenda shule za upili na msingi wanakosa kupata viwango sawa vya usalama. Unakumbuka miaka miwili au mitatu iliyopita tulikuwa na janga kubwa sana la shule za upili kuchomwa na tukaambiwa kwamba ni mambo ya mitihani na uoga kama huo. Kwa kweli Wizara ya Elimu ina maswali chungu nzima ya kujibu. La kwanza ambalo Mhe. Sossion ameliangazia sana ni itakuwa vipi tuna shule ndani ya jiji kama Nairobi ambazo bado hazijafikia viwango vinavyostahili kuwa shule zinazostahili kuwa na watoto wetu? Waziri alipofika pale jana, nilisikia akitangaza kwamba atatengeza jopo la kuangazia kile kilichotendeka mahali pale. Kwa kweli, tunajua si shule ile moja peke yake ambayo iko katika hatari. Tunajua shule nyingi ndani ya Nairobi hii na miji mingi hasa katika vitongoji. Hata katika Dagoretti yenyewe, si shule moja peke yake ambayo ina shida. Tunajua shule zimepewa ruhusa ya kufundisha watoto wetu lakini ziko katika hali duni. Bunge hili lazima lichukue hatua na pengine Kamati ya Elimu na Utafiti imshurutishe waziri kwanza aanzishe jopo la Kenya nzima kuangalia viwango vya majengo na shule zetu katika Kenya hii."
}