GET /api/v0.1/hansard/entries/953771/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 953771,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/953771/?format=api",
"text_counter": 134,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante, Bw. Naibu Spika. Kwanza, ningependa kujiunga na wenzangu waliongea hapo awali na kusema kwamba Mswada huu ni muhimu sana katika maisha yetu ya kaunti na taifa nzima. Katika Bunge la Kumi na Moja tulikuwa na Mswada huu ambao tuliufanyia marekebisho yaliyokuwa yanahitajika. Hata hivyo, kwa sababu ya wakati, hatukuweza kuukamilisha na uwe sheria. Tukizingatia zaidi, tunaona kwamba Mswada huu unaleta sura ambayo watu wa mashinani wataweza kuhusihwa kutambua watu ambao walifanya mambo ya kutambulika katika vitongoji vyao. Hii ndio sababu inaitwa County Hall of Fame. Ni ukumbi wa watu waliobobea ambao historia yao inatambulika na wale wanaoishi katika kaunti zao. Kuna majukumu katika Mswada huu ambayo nimefurahia sana. Jukumu la kwanza ni kuwa Mswada huu utahusisha kila mtu katika kaunti. Kwa hivyo, katika kaunti 47, Wakenya wote watahusishwa ili walete maoni yao. Kwa mfano, watasema ni nani aliyebobea wakati huo na ni kwa nini anafaa kutambuliwa. Hilo halitakua jukumu la mtu mmoja. Haitakua jukumu la gavana ama waziri wake wa social services . Itakua jukumu la kila mtu katika kaunti. Ukumbi wa watu waliobobea katika kaunti ni muhimu zaidi ili kuweza kufafanua historia yetu na kuwawezesha wajukuu na vitukuu kujua wale watu waliotufanya tuishi jinsi tunavyoishi. Tumeona katika mataifa ya kigeni kuna sanamu kila mahali. Kwa mfano, ukitembelea Ufaransa, Ubelgiji au Uingerezea utapata samamu. Wengine wetu hupenda kupiga picha na kusema: “Nilikua katika hii sanamu au ile katika nchi ya Ufaransa, hasa katika Mji wa Paris, na inasema hivi na vile.” Lakini hapa kwetu hicho ni kizungumkuti. Itakuwa vyema kama sisi ikiwa tutatambua mambo yaliyofanywa na wale waliotutangulia kama vile nchi zingine zinafanya. Ni vizuri kuweka historia ya walipotoka mpaka pale walipofika. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}